Mkurugenzi wa Shule ya Msingi High Mount na Sekondari ya High View Benard Kasika akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari shuleni kwake Gongo la Mboto Mwisho wa Lami, Ilala, Jijini Dar es Salaam.
…………………………….
Na Mwandishi Wetu.
Serikali imepongezwa kwa kutengeza mazingira mazuri ya elimu nchini hali ambayo imeifanya sekta binafsi kutoa mchango mkubwa kwenye eneo hilo.
Mkurugenzi wa shule za ya Msingi High Mount na ya Sekondari ya High View zilizopo Gongo la Mboto Mwisho wa Lami Ilala, Dar es Salaam,Benard Kasika, alisema jana Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Waandishi wa Habari kwamba kutokana na mazingira hayo sekta binafsi inatoa mchango mkubwa sana katika maendeleo ya elimu hapa nchini,
“Hapa tuna waalimu wawili wenye Shahada za Ualimu ambao wamepita wamesoma katika shule hii pia tuna madaktari ambao wamepita hapa na sasa wanatoa huduma mbalimbali kwa wananchi hapa chini,” alisema.
Alifanua kuwa shule binafsi pia ikiwamo anazoziongoza zimekuwa zikiibua na kuendeleza vipaji mbalimbalivya vijana na hivyo kusisaidia serikali katika eneo hilo na uibiaji na ukuzaji wa vipaji kwa vijana,
Kasika alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta elimu hapa nchini.
“Ushirikishwaji wetu kama sekta binafsi na mamlaka zinazosimamia elimu hapa nchini umeendelea kuwa mkubwa ,kwa kweli tunaipongeza serikali yetu kwa kutushirikisha hasa katika eneo la utungaji wa mitihani mbalimbali ya kitaifa,” alisema.
Alisema ndani ya kipindi hiki uhuru wa kutoa mawazo umekuwa mkubwa hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
Anatoa wito kwa mamlaka za elimu nchini ziendelee kuwapa semina mbalimbali waalimu ilikukabiliana na changamoto mbalimbali za ukiaji wa teknolojia.
“Teknolojia inakua kila siku ni vema mamlaka za elimu zikaendeleakuwapiga msasa waalimu wetu ili waende sanjari na ukuaji huo,” alisema