Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akiwasili katika Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi na
kupokelewa na Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Nayishimiye leo tarehe
06 Mei 2023. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 11 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mpango wa Amani,
Usalama na Ushirikiano kwaajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika Bujumbura nchini Burundi.