Mahakama ya hakimu mkazi wa Mkoa wa Tabora ,Imewahukumu watu wawili kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kuingia kwenye hifadhi ya Taifa bila kuwa na kibali maalum.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Jovith Katto alisema hukumu hiyo ilitakuwa fundisho kwa watu wengine wenye dhamira kama hiyo.
Hakimu huyo aliwataja watu hao kuwa ni Hamisi Omari (32) na Tobias Magazi (46) wote ni wakazi wa kata ya Ugalla katika Wilaya ya Sikonge hapa.
Katto alisema kwamba kitendo cha washitakiwa hao kuingia ndani ya hifadhi kwa kujibu wa sheria za nchini ni kosa hivyo wanastahili adhabu .
“Mahakama inasema Kimsingi kutoijua sheria sio Kinga kwa Mujibu wa Sheria za Kitaifa kwa uharifu walioufanya kwenye hifadhi hiyo ,hivyo washitakiwa alikuwa analima kwenye hifadhi bila kujua kwamba ile ni hifadhi “alisema Kato
Awali Wakili wa Serikali ukiongozwa na Flavia Francis aliambia mahakama hiyo kwamba juni 2 mwaka 2022 washitakiwa pamoja walikamatwa wakiwa kwenye hifadhi eneo tengefu la ugalla ambalo lipo katika eneo la wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora bila ya kuwa na kibali kutoka kwenye mamlaka ya usimamizi wa uhifadhi wa mazingira .
Alisema kwamba siku hiyo waliingia kwenye hifadhi na kufanya uharibifu wa mazingira kwa kupasua Mbao kinyume na kifungu namba cha sheria 18 ibara ya ndogo ya kwanza na ya 3 cha sheria uhifadhi wa mazingira sura namba 5 ya 2009 .
Flavia shitaka la pili ni kukutwa kwenye hifadhi wakiwa na mali zilizozalishwa ndani ya pori ambazo kimsingi ni mbao kinyume na kifungu namba 88 cha sheria ya misitu sura nama 14 kama ilivyolekebishwa mwaka 2002.
Shitaka la tatu wanashitakiwa ni walikutwa kwenye hifadhi wakiwa wanamiliki mali haramu za kufanyia ujangili ndani ya pori ambazo ni nyaya haramu za kutegea wanyama ,baiskeri 3 ,shoka 2 kinyume na kifungo namba 17 cha ibara ndogo cha kwanza na cha pili ikisomwa Sambamba na kifungo namba 20 ibara ndogo ya kwanza B na 4 cha sheria ya uhifadhi wa mazungira sura namba 5 ya mwaka 2009 .
Hata hivyo Washitakiwa wote waliiomba Mahakama hiyo kuwapunguzia adhabu kwani wanatengemewa na familia zao .
Wakili wa Serikali ukiongozwa na Flavia Francis waliomba Mahakama kutoe adhaba kali kwa wshitakiwa hao ili fundisho kwa watu hao