MWENGE wa uhuru umeridhia na ujenzi wa mradi wa kituo cha Mafuta NFS kilichopo Mafinga mjini mkoani Iringa na kuzinduliwa.
Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Milioni 850 unatarajia kutoa ajira za muda mrefu na ajira za muda mfupi kwa vijana zaidi ya 30.
Lengo la ujenzi wa mradi huo ni kutoa huduma bora ya mafuta kwa wananchi na vilainishi kwa ajili ya magari na mitambo kwa wakazi wa mji wa Mafinga pamoja na wasafiri na wasafirishaji.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdalla Kaim alipongeza juhudi za mwekezaji huyo na kusema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili waendelee kuwekeza katika miradi mbalimbali Nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hicho James Mwinuka ambae ni mfanyabiashara ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa kipaumbele wazawa na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli za uwekezaji.
Mwenge wq uhuru umehitimisha mbio zake mkoani Iringa katika Halmashauri ya mji wa Mafinga mei 5/2023.
Ukiwa Halmashauri ya mji wa Mafinga ulitembelea miradi 8 yenye thamani ya Bilioni 38.9.
Mwenge wa Uhuru unaendelea na ziara yake mkoani Morogoro.