Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIRC kama taasisi yenye lengo la kuendeleza na kusimamia sekta ya umwagiliaji nchini imetoa taarifa kuhusu shughuli mbalimbali inazoendelea nazo Kwa sasa ili kuboresha huduma zake.
Katika taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imesema inafanya kazi kwa bidii kuimarisha mifumo ya umwagiliaji, kuongeza uzalishaji wa mazao na kuinua hali ya maisha ya wakulima nchini kote.
Tume hiyo imewaomba wananchi wote kushirikiana nayo katika kufanikisha azma hii muhimu kwa taifa letu.
“Tunaamini kwamba kupitia ushirikiano wetu na wananchi, tutaweza kufikia malengo yetu na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo,”. Imesema taarifa hiyo.
Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imeombwa kusaidia katika kuhabarisha umma kuhusu shughuli zake za umwagiliaji na jinsi inavyofanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yake.
“Tunajitahidi kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji, na tunahitaji msaada wenu katika kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwaelimisha kuhusu juhudi zetu,” imesema taarifa hiyo.
Tume ya Imwagiliaji inashukuri Kwa Ushirikiano ambao imekuwa ikipata na inategemea kuendelea kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma kuhusu shughuli zeke.