Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komredi Kheri James,mapema leo amefanya zoezi la uzinduzi rasmi wa Bodi ya afya ya Halimashauri ya wilaya ya Mbulu.
Akizungumza na wajumbe wa Bodi hiyo Mpya, Kheri James amewapongeza kwa Kuaminiwa na amewahimiza umuhimu wa Kuyafanya Majukumu yao kwa Weledi, Ufanisi na kwa Kuzingatia Sheria, Kanuni, Miongozo na Maazimio ya Vikao vyao yanayoheshimu Misingi ya Kitaaluma katika Sekta ya Afya.
Pamoja na mambo mengine Komredi Kheri James, amesisitiza Bodi hiyo Kusimamia Hamasa ya Wananchi Katika Kufahamu na Kushiriki katika Mipango ya Afya, Kufatilia na Kubuni mbinu za kudhiti uvujaji wa mapato Katika maeneo ya huduma za Afya Kufatilia hali ya huduma za Afya Katika vituo na zahanati Kuwa tayari wakati wote kutoa Ushauri wa maboresho katika taratibu na uendeshaji wa huduma.
Kheri James pia, ameuelekeza Uongozi wa Halimashauri ya wilaya ya Mbulu kuwajengea Uwezo wa Kuyafahamu Majukumu na Mipaka yao wajumbe wa Bodi ili waweze kuifanya kazi yao kwa ufanisi.
Aidha Kheri James amewaahidi wajumbe wa bodi kuwa yeye binafsi pamoja na viongozi,wananchi na watumishi wataipatia bodi hiyo ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao.
Uzinduzi wa bodi hii ya afya ya Halimashauri ya wilaya ya Mbulu, Umehudhuriwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mbulu Mkurugenzi wa Halimashauri, Mganga Mkuu wa wilaya, Viongozi na Watumishi Waandamizi wa idara ya afya, pamoja na Wajumbe wapya wa Bodi hiyo.
Kupatikana kwa bodi hii kutaongeza ufanisi katika kusimamia sekta ya afya, na Kutapanua wigo wa Kushiriki na Kushirikiswa kwa Wananchi katika uendeshaji wa Shughuli za Afya katika Maeneo yao.