NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya Mfuko Bora miongoni mwa Taasisi
za Bima na Fidia wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Afya na Usalama
Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro ambapo mgeni rasmi alikuwa
ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Profesa Joyce Ndalichako.
WCF
imetwaa tuzo hiyo kwa kuwa na Sera nzuri
ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika Sekta ya Bima na Fidia kwa Wafanyakazi
wakati wa Kilele cha Maonesho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa
Kazi ambapo kitaifa imefanyika mjini Morogoro.
Kilele
cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi
hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine
duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha
uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi
ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni
kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”.
Mkurugenzi
Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu), Profesa
Joyce Ndalichako.
Akizungumza
baada ya kutwaa tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba WCF, Dkt. Abdulsalaam
Omar alisema Tuzo hiyo ni faraja kwa Wafanyakazi na Mfuko kwa ujumla imeonyesha
jinsi mifumo ya kudhibiti ajali na magonjwa mahali pa kazi ni madhubuti.
“Hii
inatupa matumaini na inatupa moyo zaidi kuendelea kuboresha maeneo ya kazi na
kwakuwa WCF ni mdau mkubwa katika masuala haya hatuishii hapa tu kwa wafanyakazi
wetu bali kwa wafanyakazi wengine ambao ni wadau wakubwa wa Mfuko.” Alifafanua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro leo Aprili 28, 2023.
kudumu ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya jamii, Mhe. Fastma Tawfiq (kulia kwa Profesa Ndalichako), Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (mwenye koti jeusi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko huo baada ya kutwaa tuzo.
Usalama mahali pa Kazi WCF, Bi. Naanjela Msangi,