Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
April 28
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemhukumu Dickson Chilongola (37) ,mkazi wa Zegereni – Mlandizi ,Kibaha Mkoani Pwani, kifungo cha maisha jela ,viboko 12 pamoja na kulipa fidia ya sh.milioni 2 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 10 .
Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 13/2023 imetolewa April 27, 2023 na Hakimu Judith Lyimo wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha wakati kesi ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.
Akisoma hukumu hiyo baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Judith Lyimo alieleza , amemtia hatiani mshtakiwa huyo kwa Mujibu wa kifungu 130 (1), (2) (e) na kifungu 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Aidha katika hukumu hiyo ilielezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 01/02/2023 majira ya usiku huko mtaa wa Zegereni, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi .
Alieleza,mtuhumiwa aliingia chumbani kwa mtoto huyo kisha kumfanyia kitendo hicho cha kikatili.