Daktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja Dkt.Sabra Salum Machano akichangia mada wakati wa mafunzo ya uhamasishaji lishe kwa Waandishi wa Habari yaliyofanyika Kidongo Chekundu Zanzibar.April 28,2023.
Mkuu wa Kitengo cha Lishe Asha Hassan Salmin akizungumza wakati alipokua akiwasilisha taarifa ya utafiti wa Afya na lishe kwa Waandishi wa Habari,wakati wa mafunzo ya lishe kwa Waandishi hao yaliyofanyika Kidongo Chekundu.
…………………………
Na Rahima Mohamed Maelezo
Jamii imetakiwa kuwapatia chakula bora mama wajamzito ili kuondokana na tatizo la upungufu wa damu mwilini wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na wajawazito Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Zeyana Abdul-azizi wakati alipokuwa akitoa mafuzo kwa waandishi wa habari huko katika hospitali ya Kidongo chekundu.
Amesema tatizo la upungufu wa damu ni kubwa ambalo limekuwa likiwaathirika zaidi wanawake hasa wajawazito wakati wa kujifungua ndio wahitaji wa huduma ili kuokoa maisha ya mama na mtoto
Ameeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi machi jumla ya kina mama 903 wamegundulika na matatizo ya upungufu wa damu kiwango ambacho kikubwa na kupelekea kuwapatia waginjwa kidogo kutokana na ufinyu wa huduma hiyo.
Amefahamisha kuwa kati ya wagonjwa hao waliolazimika kuongezewa huduma ya damu ni wagonjwa 75 ukilinganisha na ufinyu wa upatikanaji wa damu benki ya damu.
Dr. Zeyana ameomba jamii kujiandaa kabla na baada ya mama kupata ujazito kutumia vrutubisho vianavyoasaidia kujikinga na upungufu wa damu wakati wa kujifungua.
“Naiomba jamii ijiandae wakati mama anapotaka kubeba ujauzito tunashauri miezi 6 kabla mama watumie virutubishi ambavyo vitawasaidia kujikinga na tatizo la upungufu wa wakati wa kujifungua”, alieleza Dr. huyo.
Hata hivyo amewasisitiza kina mama na kina baba kuhudhuria kliniki kikamilifu kupata ushauri nasaha na kuanza tiba mapema ili kuepukana na tatizo la ukosefu wa damu wakati wa kujifungua ili kunusuru maisha ya mama na mtoto.
Nae Afisa Lishe Wilaya ya Kaskazini A Omar Saleh Machano amesema upungufu wa damu ni tatizo la kiafya ambalo huathiri zaidi watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa na wajawazito ambayo husababisha matokeo mabaya ikiwemo kujifungua kabla ya wakati, upungufu wa maadini na kupelekea vifo zaidi kwa kinamama.
Afisa huyo ameisisiza ulaji jamii kuzingatia makundi sita ya vyakula ili kujenga afya bora pamoja na kuwaomba waandishi kuhamasisha jamii kujenga mazingira wezeshi ya kuimarisha lishe na mtindo bora wa maisha pamoja na ujio wa program ya utoaji dawa za kuongeza damu.