Mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge akifungua Mkutano Mkuu wa 29 wa Chama Kikuu cha ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) uliofanyika leo tarehe 25/4/2023 Mkoani Pwani
…..
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.
Mkoa wa Pwani umezalisha tani 18 za zao la Ufuta na kuingizia wakulima sh. Bilion 58.5 kwa msimu wa mwaka 2022/2023.
Akifungua Mkutano Mkuu wa 29 wa Chama Kikuu cha ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) , Mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge alipongeza jitihada hizo za Uzalishaji wa mazao ya Korosho na Ufuta ambapo Mkoa umezalisha Tan 12 za Korosho, asilimia 96.3 Korosho Daraja la kwanza na Ufuta Tan 18.
Aidha Kunenge, amemtaka Katibu Tawala Mkoa kutoa utaalamu kwa Chama kikuu hicho kwa kupitia mnyororo wa thamani wa mazao ya Ufuta na Korosho ili kutatua Changamoto.
Vilevile amekitaka Chama hicho kupanua Wigo wa kusimamia mazao mengine yanayokubalika Pwani.
Amewataka kutumia kikao hicho kufanya tathmini ya Chama Chao kama kinatekeleza Yale yaliyokusudiwa.
Mkoa wa Pwani umeshuka kwa uzalishaji upande wa zao la korosho kutoka tani 15 msimu uliopita hadi tani 12 kwa mwaka 2022/2023 licha ya kupanda kwa ubora wa korosho Daraja la kwanza kutoka asilimia 72 hadi 96.3