Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nachingwea James Chacha akizungumza na wachimbaji wa madini katika mgodi wa Nditi juu ya umuhimu wa kutunza amani
………
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
JESHI la Polisi wilaya ya Nachingwea limewataka wachimbaji wa madini katika mgodi wa Nditi kuhakikisha wanalinda amani na utulivu ili shughuli za uchimbaji wa madini uendelee kwa amani.
Akizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo kwenye mgodi wa Nditi,Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nachingwea James Chacha alisema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuilinda na amani na utulivu uliopo kwenye mgodi huo.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi wilaya ya Nachingwea limepokea taarifa za kutishiwa watu bastola na mhindi hivyo wamelichukua na wanalifanyia uchaguzi wa haraka jambo hilo kwa kuwa ni kinyume na sheria za nchi.
OCD Chacha alisema kuwa hakuna mwananchi yeyeto yule mwenyewe ruhusa ya kuwatishia bastola au kupiga risasi hadhara bila kuwa ruhusa au unakumbana na madhara hivyo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa mapema waposikia tena Milio ya risasi.
Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nachingwea James Chacha alimalizia kwa kuwataka wachimbaji wadogo wadogo kuacha kuiba madini ya wachimbaji wakubwa kwa kufanya hivyo kunawapelekea hasara wachimbaji hao
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo aliagiza kujengwa kwa kituo cha Polisi katika machimbo ya madini ya Nditi ndani ya siku 14 ili kuondoa migogoro inayoendelea katika mgodi huo.