Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja akizungumza na waandishi na wahariri wa vyombo vya habari wanaoshiriki katika kikao kazi na wizara hiyo huku akionesha mpango kazi wa wizara hiyo kuhusu mawasiliano kikao, Kazi hicho kinachofanyika hazina ndogo ya Wizara ya Fedha jijini Arusha.
……………………..
Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imesema itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma pamoja na kuhakikisha wanajua ukweli wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya Taifa.
Akizungumza na wahariri wa vyombo va habari Aprili 24, 2023 Jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi na wahariri hao, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja, amesema kuwa wataendelea tutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari kutokana ni wadau muhimu katika kufikia malengo tarajiwa.
“Tumekuwa tukifanya kazi pamoja na nyinyi kwa kipindi kirefu katika utendaji wetu kwa lengo kuendelea kuelimisha jamii kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali yenye tija kwa jamii na Taifa “amesema Mwaipaja.
Amesema Wizara imekuwa wakitafuta fedha kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo, huku akieleza kuwa vyombo vya habari vimekuwa mstali wa mbele katika kutoa taarifa kwa katika kufanikisha mipango.
Amesema kuwa wamekuwa wakiwategemea kwa sababu hawawezi kuifikia jamii bila kupitia waandishi wa habari ambao mara kwa mara wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Ili tuweze kufanya vizuri mnapaswa kuwa uwelewa mpana kuhusu wizara ya fedha pamoja na kujua masuala ya kiuchumi yanakwendaje na inakuwaje katika utekelezaji wake” amesema Mwaipaja.
Ameeleza kuwa uchumi katika maisha ya kila mtu ni jambo la kwanza , hivyo waandishi wa habari ni watu muhimu katika kutoa elimu jamii.
Hata hivyo amebainisha kuwa kupitia kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari wanaendelea kutoa elimu juu ya Wizara pamoja na kutoa muongozo kwa wastaafu pamoja na utekelezaji wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja akifafanua jambo katika kikako kazi Cha wahariri wanaofanya kazi Kwa karibu na Wizara ya Fedha kinachofanyika jijini Arusha kulia ni Benny Mwang’onda Mhariri Mkuu Msaidizi kutoka AZAM MEDIA na Mwenyekiti wa Kikao hicho na kushoto ni Mhariri Mkuu wa Clouds na Katibu wa kikao hicho Joyce Shebe.
Mhariri Mkuu wa Clouds na Katibu wa kikao hicho Joyce Shebe akizunguma katika kikao kazi hicho huku Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja akifurahia.
CPA(T) Kuluthum Slaa Mhasibu Wizara ya Fedha na Mipango kushoto na Ramadhan Kissimba Afisa Habari Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja hayupo pichani wakati akifungua kikao kazi hicho.
Picha mbalimbali ikionesha wahariri wa vyombo vya habari wakishiriki katika kikaokai hicho.
Eva Ngowi Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango akifuatilia hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi hicho.
PIcha ya pamoja.