Mtaalamu wa Mashirikiano COSTECH Promice Mwakale wakati akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya kuongeza Thamani kwenye Teknolojia ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Intermech Engineering LTD Morogoro Mhandishi Peter Chisawillo akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya kuongeza Thamani kwenye Teknolojia ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia leo jijini Dar es salaam.
Mmoja wa Washiriki katika warsha hiyo Kiko Kiwanga kutoka Morogoro Chisawillo akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya kuongeza Thamani kwenye Teknolojia ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia leo jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja wadau wabunifu ambao wamehudhuria katika warsha ya kuongeza Thamani kwenye Teknolojia ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia leo jijini Dar es salaam.(picha na Mussa Khalid)
……………………
NA MUSSA KHALID
Tume ya Sayansi na Teknolojia –COSTECH imesema itaendelea kuongeza thamani ya kutengeneza bunifu na teknolojia kwa wataalamu kuongea na wabunifu ili kusaidia kuboresha teknolojia zenye manufaa.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mtaalamu wa Mashirikiano COSTECH Promice Mwakale wakati akizungumza katika warsha ya kuongeza Thamani kwenye Teknolojia ambayo imeambatana na maonyesho ya bidhaa ambazo zimeweza kufanyiwa kazi na vyuo vya elimu kwa kushirikiana na wabunifu.
Mwakale amesema warsha hiyo ni muhimu kutokana na uwepo wa bunifu nyingi ambazo zimeweza kufanyiiwa na kuongea tija katika viwango vya kitaifa na kimataifa
Awali Akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni ya Intermech Engineering LTD Morogoro Mhandishi Peter Chisawillo amesema wamefanikiwa kubuni na kuiunda Mashine ambazo zinasindika mazao ya Kilimo hasa kwa kukausha mihogo.
Naye Mmoja wa Washiriki katika warsha hiyo Kiko Kiwanga amesema majadiliano ambayo wameyafanya wamejifunza pia kuangalia namna ya kuilinda Teknolojia kabla haijapelekwa kwenye Jamii.
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu zilizoanza tarehe 19 – 21 Aprili 2023 na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 103 toka sekta mbalimbali zinazoendelea kufanyika kupitia Ukumbi wa Mikutano wa COSTECH uliopo Sayansi (Kijitonyama) – Jijini Dar es salaam inakata kiu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam na kutumika kama jukwaa la kutangaza bidhaa za kitafiti na bunifu kwa wajasiriamali, Wabunifu na Taasisi mbalimbali kutumia fursa hiyo adhimu ya kujitangaza na kubiasharisha bidhaa hizo ili ziweze kuwafikia wananchi na kuwaletea maendelo kwa haraka kiuchumi na kijamii nchini.