Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. BENO MALISA Aprili 20, 2023 amewataka
madereva wa vyombo vya moto kubadilika kufuatana na hali ya kijiografia yam
ilima, miteremko pamoja na hali ya hewa ya Mkoa wa Mbeya yenye mvua na
ukungu kwa kuhakikisha wanafuata na kuzingatia sheria na alama za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Ameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
barabarani Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika Stendi ya kabwe Jijini mbeya,
ambapo Mhe.BENO MALISA alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Mhe.Comrade JUMA ZUBERI HOMERA.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mhe.malisa amelipongeza Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa wakati wa
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa mkoani
mwanza.
Aidha amepongeza jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
kwa kushirikiana na kamati ya usalama barabarani katika kuzuia na kudhibiti
ajali za barabarani kwani kitakwimu ajali zimepungua ukilinganisha na mwaka
2022.
Sambamba na hilo, Mhe.Malisa amempongeza na kumshukuru Mhe.Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha
zaidi ya Bilioni mia moja kwa ajili ya ujenzi na utanuzi wa barabara ya
TANZAM Jijini Mbeya.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga ambaye pia
ni mlezi wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Mbeya ametoa onyo kwa
watu wanaong'oa na kuharibu alama za usalama barabarani na kwenda kuuza
Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
S. L. P. 290,
MBEYA