Marafiki wa Rais Samia (Friends Of Samia) wakiongozwa na Mtangazaji Mwijaku na Msanii Alikiba, Maua Sama, na Gea Habib wameshiriki Dua maalum ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kushiriki iftar ya pamoja watoto wenye mahitaji maalum katika kituo cha Ijango Orphanage Center kilichopo Sinza jijini Dar es salaam.
Wakizungumza kwenye Iftar hiyo ya pamoja marafiki hao wa Mama Samia (Friends Of Samia), wamewaomba watoto hao kuendelea kumuombea Rais wa Sama Suluhu Hassan pamoja na Wasaidizi wake ili waendelee kuwaletea maendeleo Wananchi wote.
Aidha Marafiki hao wa Rais Samia wamekabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo mchele, Unga, Sabuni, Maji, Mafuta kwa ajili ya watoto hao kusherehekea vyema Sikukuu ya Eid Elfitr