Kamati ya Usalama Wilaya ya Same imelazimika kuingilia kati na kusitisha mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Empower Tanzania kwa walimu wa shule za msingi na Sekondari wilayani humo Mafunzo ya Afya ya Jamii, Afya ya Uzazi na Mahusiano , baada ya kubaini Dosari ikiwemo vitabu vinavyo tumika kufundishia kuwa na viashiria vya maadili yasiyofaa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo,Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema katika ufuatiliaji na Vyombo vya Usalama wamebaini kuna mapungufu makubwa ikiwemo baadhi ya Picha na maneno yaliyomo kwenye vitabu vinavyo tumiwa na Taasisi hiyo kufundishia kuwa na viashiria vya kuhamasisha mambo yasiyo faakwa wanafunzi.
Mbali na kusitisha mafunzo pia kamati hiyo imemtaka Mkurugenzi wa taasisi hiyo kusitisha shughuli zote zinazohusu Mafunzo ya Afya ya Jamii,Afya ya Uzazi na Mahusiano kwa wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari katika wilaya ya Same mpaka itakapo amuliwa vinginevyo akimkata pia mkurugenzi huyo kusaidia vyombo vya usalama kutoa ufafanuzi wa masuala hayo.
Amesema vitabu vilivyo bainika kutumiwa na Taasisi hiyo huenda ni kati ya vile vilivyo tolewa katazo na serikali kutosambazwa wala kutumiwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini hasa kwenye taasisi za Elimu na kwamba vitabu vyote vichukuliwe kwa ajili ya uchunguzi zaidi, pia kufanyiwa marekebisho kabla ya kutumika kama itafaa.