Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amewataka maafisa wa sekta ya ardhi kumaliza kero na migogoro ya ardhi ya wananchi katika maeneo kuanzia ngazi za chini kabla ya kufika ngazi za Wilaya, Mikoa na Taifa.
Naibu Waziri Pinda amesema hayo wakati wa Mahafari ya 41 ya Chuo cha Ardhi Morogoro yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho nakuhudhuliwa na Wahitimu takriban 300 waliofuzu katika fani mbalimbali za sekta ya Ardhi.
’Zuieni maandamano ya migogoro ya ardhi kwenda kwa wakuu wa wilaya na mikoa. Inasikitisha kuona mwananchi anafuatilia hati mwaka mzima au kwenda ngazi ya Wizara hadi Ikulu kufuatilia Migogoro wakati Wizara ina watumishi kuanzia ngazi ya Mikoa, tukikuta afisa analimbikiza kesi za ardhi na kusababisha zinaenda kwa wakuu wa wila na mikoa tutamchukulia hatua.’’ Alisema Naibu Waziri Pinda.
Ameonya kuwa kumekuwa na malalamiko malalamiko ya Wananchi hayatakiwi kwenda kwa viongozi wa wajuu wa Serikali kwani wao sio wataalamu wa ardhi masuala ya Ardhi kwani changamoto hizo ni bora zikatatuliwa na wataalam wenye ujuzi katika fani hiyo.
Aidha, Pinda ameonya tabia ya baadhi ya wataalam sekta ya ardhi na kuwataka kuacha tabia mbaya nakuepuka vitendo vya rushwa akionya kuwa maaana ya rushwa ni kutenda kazi bila kuzingatia matakwa ya kisheria.
Akioneshwa kusikitishwa na vitendo vya rushwa katika Sekta ya Ardhi Nchini Naibu Waziri Pinda amesema ni lazima vyuo vya ardhi vianzishe mtaala wenye somo la maadili ndani yake ili wanachuo hao watakatakapoanza kuitumikia jamii wasiendelee na changamoto ya rushwa inayoigubika sekta hiyo.
Pinda ameagiza Wakurugenzi katika Wizara yake waangalie uwezekano wa kutumia wahitimu wapya sekta ya ardhi ili wapewe kazi katika miradi yote inayoendelea Wizarani ili kuwajengea uwezo wa kufanyakazi kiufanisi mara watakapopata ajira rasmi.
Akiongelea kuhusu mikakati ya uendelezaji chuo Waziri Pinda amewataka bodi ya chuo hicho kuanza mara moja hatua za ujenzi wa miundombinu mipya hivyo kuwataka kufika Wizarani ili kuwasilisha andiko lao ili hatua zianze kuchukuliwa.
Pinda ameongoza kuwa Chuo hicho kimekuwa na miundombinu ya zamani na hivyo mahitaji ya kupata miundombinu ya kufundishia haiepukiki na kuhaidi kuwa suala hilo wanaenda kulifanyia kazi.