Mjumbe wa Kamati ya Michezo Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Bw. Imran N. Jaffer akikabidhi vitu mbalimbali ikiwemo unga wa sembe, ngano, sukari, sabuni, maji, juice kwa uongozi wa Kituo Cha Kulea Watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kata ya Hananasif, Halmashaur
…………………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mjumbe wa Kamati ya Michezo Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Bw. Imran N. Jaffer ametembelea Kituo Cha Kulea Watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kata ya Hananasif, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Lengo la kutembelea kituo cha Maunga kwa ajili ya kuwafariji watoto kwa kuwapatia mahitaji ya vitu mbalimbali ikiwemo unga wa sembe, sukari, mchele, mafuta ya kupikia, sabuni, unga wa ngano, juice, maji.
Akizungumza na watoto wa kituo Cha Maunga Imran N. Jaffer amesema kuwa Jumuiya ya wazazi Chama Cha CCM ipo karibu na watoto kwa ajili ya kuwasaidia ili kuhakikisha wanafikia malengo tarajiwa katika maisha yao.
“Msijione mpo peke yenu, sisi wazazi tupo pamoja na nyinyi muda wote ili kuhakikisha tunawasaidia na kufikia ndoto zenu” amesema Jaffer.
Hata hivyo amewataka wasome kwa bidii jambo ambalo litawasaidia kufikia ndoto zao ambazo wamekusudia, huku akiwasisitiza kujiamini ni njia muhimu ya kufanikiwa katika maisha.
Imran N. Jaffer katika kufanikisha tukio la kutembelea kituo Cha Maunga ameongozana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Bw. Makame Ally, Katibu Mwenezi Kata ya Hananasif Bw. Abdallah Zaydii pamoja na Bw. Kessy Myambo.