Adeladius Makwega-MWANZA
Wafanyakazi wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya, mkoani Mwanza Aprili 13, 2023
wamemchagua mkufunzi Denis Kayombo kuwa mfanyakazi bora kwa mwaka huu katika
uchaguzi uliwakusanya wafanyakazi wote wa kada mbalimbali kuelekea Siku ya Wafanyakazi
Duniani, Mei Mosi , 2023.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi mwalimu Kayombo alisema,
“Ninawashukuru sana, maana niliamka asubuhi sikuwa na ili wale lile
kujua kuwa leo nitachaguliwa kuwa mfanyakazi bora. Asanteni sana
kwa kuwa mmeona ninatosha na ninafaa. Mimi na wezangu
tuliokuwa katika kinyang’anyiiro hiki sote ni bora. Nilipokuwa napiga
kura nilijipigia mwenyewe kwa kuwa nilipendekezwa tu, nikiogopa
kukosa kura kabisa, angalau nipate kura hata moja, lakini kumbe
wengine mmenipigia! Tushirikiane kukipeleka mbele chuo chetu na
kuyafanikisha maslahi mapana ya michezo na taifa letu.”
Katika uchaguzi huo mkufunzi Silveli Hema alipata alipata 6.7% ya kura zote, mkufunzi Idd
Luswaga alipata 33.3% ya kura zote na huku mkufunzi Denis Kayombo aliyeshinda alipata 60%
ya kura zote.
Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo hayo mwakilishi wa TUGHE katika Baraza la
Wafanyakazi Bi Rita Samweli alisisitiza,
“Tumeshafanya uchaguzi na tumempata yule ambaye tunamuona ni
sahihi kupata nafasi hii, ninachoomba tuendelee kushirikiana,
tuendelee kufanya kazi ili tuone tunafanyaje kwa mwenzetu
aliyeshinda. Tunawapongeza wote watatu mliopigiwa kura, nyinyi ni
wafanyakazi wetu bora lakini jina moja ndilo linalotakiwa.”
Kikao hicho cha uchaguzi kilihitimishwa kwa mwakilishi wa wafanyakazi wa Chuo Cha
Maendeleo ya Michezo Malya katika Baraza la Wafanyakazi Wizarani mkufunzi mkuu Joachim
Maganga kutoa mrejesho wa Kikao cha Baraza la Wafanyakzi la Machi 2023.