Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea
Tanzania-TFRA Dkt Stephen Ngailo (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya
Ruzuku kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania-TFRA Louis Kasera (kulia)
wakizungumza na jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea
Tanzania-TFRA Dkt Stephen Ngailo akitoa taarifa ya maandalizi ya msimu wa
Kilimo 2023/2024 sambamba na mikakati ya kuimarisha upatikanaji na usambaji wa
Mbolea katika mkutano wake leo na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa
Mbolea Tanzania-TFRA Louis Kasera akizungumza na waandishi wa habari akitolea
ufafanuzi mikakati ya kuimarisha upatikanaji na usambaji wa Mbolea.(Picha na
Mussa Khalid)
……………
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania-TFRA imetoa tahadhari kwa watakaojaribu kuhujumu mpango wa utoaji wa Mbolea ya Ruzuku kwa wakulima kwa njia mbalimbali za udanganyifu ikiwemo kutoa taarifa zisizosahihi.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt Stephen Ngailo wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya msimu wa Kilimo 2023/2024 sambamba na mikakati ya kuimarisha upatikanaji na usambaji wa Mbolea.
Dkt Ngailo amesema kuwa malengo yao mpaka kufika msimu wa 2024/2025 kuhakikisha wanasajili wakulima wapatao Mill 7 katika nchi nzima.
Aidha Dkt Ngailo amesema TFRA itaendelea kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ili kuhamasisha wakulima kwa njia mbalimbali kujisajili Kwenye Mfumo wa Ruzuku kufuatia utekelezaji na utatuzi wa changamoto mbalimbali Wwa utekelezaji wa Mpango huo.
“Katika kutekeleza Azam ya serikali Mamlaka Kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo,sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa inaendelea kusajili wakulima, kutumia Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC),kuandaa Ramani ya Mtandao wa usambazaji wabolea nchini na kuainisha maeneo ambayo hayana wafanyabiashara na kuchukua hatua stahiki”amesema Dkt Ngailo
Kuhusu kuongeza uzalishaji ndani ya nchi Dkt Ngailo amewataka wakulima nchini kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi kujisajili kwa wakati ili kuwawezesha kunufaika na mbolea ya ruzuku kwa wakati kama ilivyopagwa na serikali.
Amesema katika msimu wa 2023/2024 usajili wa wakulima unalenga kusafisha au kuhuisha taarifa za mkulima na kufikia maeneo ambayo hayakufikiwa msimu wa 2022/2023
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku Louis Kasera amesema kuwa mipango yao ni kuhakikisha kila mkulima anapata kadi yake ili aweze kutambulika kwa urahisi mashamba aliyonayo.
Pia amewasihi wakulima kutoa taarifa sahihi na kuepukana na udanganyifu kwani atakayebainika atachukuliwa hatua kali.
Hata hivyo serikali imesema itahakikisha kuwa ifikapo Julai mosi mwaka huu mbolea zote zipatikane katika maeneo yote nchini ili kuwawezesha wakulima kuanza shughuli za kilimo mapema.