Mpiga Picha mkongwe ambaye ameitumikia serikali kwa kipindi kirefu akiwa mfanyakazi wa Magaeti ya serikali na kisha Mpiga picha wa Ikulu Bw. Muhidin Issa Michuzi ametoa mafunzo na uzoefu wake katika kazi ya kupiga picha kw maofisa habari wa Mahakama ya Tanzania nchini inayofanyika kwenye kituo Jumuishi Cha utoaji haki mkoani Morogoro leo Jumatatu Aprili 3, 2023, semina hiyo itafanyika kwa siku 5 ina lengo la kuwajengea uelewa wa namna ya kupiga picha za viongozi na matukio mbalimbali katika utumishi wao kama maofisa habari wa mahakama ya Tanzania.
Maofisa Habari wa Mahakama Kuu ya Tanania nchini wakimsikiliza kwa makini Mpiga Picha mkongwe Bw. Muhidin Issa Michuzi wakati akitoa mafunzo na uzoefu wake katika kazi ya kupiga picha kwa maofisa habari wa Mahakama ya Tanzania nchini inayofanyika kwenye kituo Jumuishi Cha utoaji haki mkoani Morogoro leo Jumatatu Aprili 3, 2023
Mary Gwera Ofisa Habari Mwandamizi wa Mahakama ya Tanzania kulia pamoja na maofisa wenzake wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyokuwa yakitolewa na Mpiga picha mkongwe nchini Bw. Muhidin Issa Michuzi mkoani Morogoro.
Bw. Muhidin Issa Michuzi akifurahia jambo wakati alipokuwa akitoa mafunzo na uzoefu wake katika kazi ya kupiga picha kwa maofisa habari wa Mahakama ya Tanania nchini inayofanyika kwenye kituo Jumuishi Cha utoaji haki mkoani Morogoro leo Jumatatu Aprili 3, 2023 katikati ni Dkt. Patricia Kisinda Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga na mmoja wa maafisa habari wa Mahakama ya Tanzania Bi.Ridia Churi.