Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mh. Paul Ngwembe akifungua semina ya waandishi wa habari na wahariri inayofanyika Katika kituo Cha utoaji haki jumuishi Morogoro leo Jumatatu Aprili 3, 2023, itakayofanyika kwa siku 5 ambayo ina lengo lakuwajengea uelewa wa namnaya kuripoti habari za mahakama.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Morogoro Christina Mbando akimkaribisha Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mh. Paul Ngwembe ili kufungua semina hiyo.
Dkt. Patricia Kisinda Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga akieleza mambo kadhaa kuhusu mafunzo hayo kwa waandishi wa habari yanayofanyika Katika kituo Cha utoaji haki jumuishi Morogoro leo Jumatatu Aprili 3, 2023.
Baadhi ya wahriri na waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo
Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Morogoro Mh. Paul Ngwembe akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa seina hiyo na baadhi ya viongozi wa mahakama kanda ya Morogoro kulia ni Dkt. Ptricia Kisinda Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga na kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Morogoro Christina Mbando mara baada ya kufungua mafunzo hayo.
Na Farida Mangube Morogoro.
MAHAKAMA ya Tanzania imetoa wito kwa wadau wegine wa mahakama hiyo kutumia mifumo ya Tehema ili kurahisha usikilizwaji wa mashauri ili kuendana na kasi ya muhimili huo uliojitanabaisha kwenye matumizi ya Teknolojia .
Hayo yametanabaishwa leo tarehe 3 Aprili 2023 kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari za mahakamani,wahariri na maafisa habari yanayofanyika mkoani Morogoro yenye lengo la kuwapa uelewa wanahabari juu ya mwenendo mahakama kwenye matumizi ya Teknolojia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Morogoro Paul Ngwembe, amesema kuwa mahakama imepiga hatua kubwa kwenye matumizi ya Tehama kwa kumiliki mifumo mbalimbali inayowezesha kazi zake kirahisi hivyo ametoa wito kwa wadau wengine kuendana na mwendo huo.
“Nitoe wito kwa wenzetu ,Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP), Mawakili wa Serikali, na Mawakili wa kujitegemea kuiga mfano wa Mahakama katika masuala ya Teknolojia ili kusudia twende pamoja mahakama haiwezi kutekeleza majukumu yake ikiwa wenzetu wadau muhimu wakiwa nyuma tunataka na wananvchi waijue vizuri mifumo hii ili waweze kuendesha mashaufi yao bila gharama kubwa” amesema Jaji Ngwembe.
“Mifumo hiyo ni pamoja Mfumo wa Tanzili ambao huchapisha uamuzi, sheria na kanuni umefanya vizuri na kuifanya mahakama ya Tanzania kuwa ya kwanza Duniani kutembelewa na watu wangi kwa asilimia 82.7 ambapo nchi inayoifuta tanzania yenye mfumo kama huo ana asilimi 2.4 hapo unaona kwa namna ambavyo tulivyokuwa kinara” Jaji Ngwembe.
Amesema kuwa mfumo huo unaonyesha hukumu kwa uwazi pale ambapo inapotolewa pia unaonyensha mashauri takribani 32 yanayoendelea duniani na kwamba ni mfumo rahisi kutumia nan hauna gharama kubwa .
Jaji Ngwembe amesema kuwa Mfumo mwengine ni JSDS 2) mfumo wa kieletroni wa kusajili mashauri na kesi mbalimbali bila kufika mahakamani na kusikilizwa.
“Tangu tumekuwa na mfumo huu tumerahisisha usikilizwaji wa mashauri huhitaji kufika mahakamani unaweza kufungua shauri kwa njia ya tehama na shauri likasikilizwa mfumo huu unakwenda sambamba na mfumo usikizwaji wa kesi kwa njia ya video (Video Confrence)”amesema Jaji Ngwembe.
Jaji Ngwembe amesema Mfumo wa tatau unawasajili na kuwatambua mawakili wa mahakama ” umeleta matunda makubwa kwa mahakama kwa kuwezesha kutekeleza majukumu yake na kuwafichua mawakili vishoka ambapo walikuwa wanajifanya wanasheria, mahakimu au mawakili bila kuwa na sifa zinazowezesha kuwa mawakili, hivyo mfumo huo umepunguza kwa kwa kiasi kikubwa uhalifu wa kisheria”
Amesema kuwa sheria hamruhusu mtu asiye na sifa za kuwa wakili kufanya kazi ya uwakili na kwamba mwananchi kupitia mfumo huo atamtambua mtu mwenye sifa ya kufanya kazi ya uwakili kwa kuwa mfumo huo unaweka picha na jina la wakili anayestahili kufanya kazi.
Amesema kuwa mfumo wa nne unaowezesha mahakama kufanya kazi zake ni ule mfumo wa kusikiliza mashauri kwa njia ya video yaani Video Conference ambapo mfumo huo unanganisha Magereza, mahakama, wakili, Ofisi ya DDP .
“Mfumo huu unaweza kusiliza shauri bila kufika mahakamani mimi nimesikiliza mashauli na mashahidi kutoka Kigoma , Mtwara, au Sumbawanga nikiwa hapa Morogoro shahidi anatoa ushahidi wake mpaka anamaliza na tunamuuliza maswali mpaka tunamaliza, mfumo huu wananchi wakiuelewa vizuri kutasaidia kupunga gharama za kuendesha mashauri ” amesema Jaji Ngwembe.
Amesema kuwa Mahakama haijishia hapo imeongeza ufanisi wa utoaji elimu ya sheria kwa wananchi kwa kuanzisha kituo cha kupokea simu za wananchi ili kuwafahamisha masuala mbalimbali ya kisheria “wananchi wanapiga simu moja kwa moja na hupokelwa kwenye hiyo Call Center na huuliza masuala ambayo hujibiwa moja kwa moja ” amesema Jaji Ngwembe.