Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akitengua maamuzi batili ya Serikali ya Kijiji Cha Naipingo kata ya Naipingo Wilayani humo yaliyomuondosha madarakani Christopher Ngunyali aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji hicho

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Naipingo wakimsikilizaM wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akitengua maamuzi batili ya Serikali ya Kijiji Cha Naipingo kata ya Naipingo Wilayani humo yaliyomuondosha madarakani Christopher Ngunyali aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji hicho

………………………………………
Na Fredy Mgunda,
Nachingwea
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametengua maamuzi batili ya Serikali ya Kijiji Cha Naipingo kata ya Naipingo Wilayani humo yaliyomuondosha madarakani Christopher Ngunyali aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya aliyefika Kijijini hapo baada ya kupokea malalamiko yaliyowasilishwa Kwa njia ya barua na mtendaji wa kata ya Naipingo, Alisema utaratibu ulikiukwa ikiwemo kutokuwapo Kwa vikao halali vya kumuondosha madarakani kiongozi huyo aliyechaguliwa na Wananchi.
Moyo alisema kuwa kuwa serikali ya kijiji hicho inajumla ya wajumbe 25 ambao wanaweza kutoa maamuzi yoyote ya serikali ya kijiji lakini katika kujadili swala la mwenyekiti walikuwepo wajumbe kumi na moja (11) jambo ambalo limesababisha kuondelewa mwenyekiti kwenye nafasi hiyo.
Alisema kuwa hayapingi malalamiko hayo bali anachopinga ni namna ambavyo utaratibu uliotumika kumuondoa mwenyekiti kwenye nafasi ya uongozi.
Moyo alisema kuwa amemrejesha kwenye nafasi ya uongozi kwa kuwa Kikao kilichofanywa na wajumbe waliomuondosha hakikuwa kikao halali kwani mwenyekiti wa kikao hicho hakuwa miongoni mwa wajumbe huku akidi haikutimia ili kufanya maamuzi.
Alisema kuwa wajumbe wanatakiwa kurudi kwenye vikao halali ili kuweza kumuondosha mwenyekiti huyo kama wanataka kwa kufuata utaratibu unaotakiwa kama vile wajumbe kufikia robo tatu ya wajumbe,wapige kura au chama ndio kiamue kufuta uanachama.
Moyo alisema kuwa chama cha mapinduzi kata ya Naipingo hawana mamlaka ya moja kwa moja kumuondoa madarakani mwenyekiti huyo, mwenye mamlaka ya kumuondosha mwenyekiti ni mkuu wa wilaya kwa kufuata sheria na kanuni za nchi.
Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Naipingo Anjeluisi Chinguile alisema kuwa chama kilifuata taratibu zote zinazotakiwa lakini tatizo lipo kwa uongozi wa serikali ya kata.