Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee PIC), Augustino Vulu, akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembea mradi huo wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (R3R2) katika vijiji vya Irisya, Masutianga na Munyu vilivyopo Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida, Aprili Mosi, 2023. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee
PIC) imewapongeza Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) kwa mradi wa usambaji wa
a umeme katika vijiji vitatu vilivyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida..
Vijiji vilivyonufaika katika mradi huo ni Munyu, Irisya na Masutianga vyote
vikiwa Kata ya Irisya wilayani humo.
Wajumbe hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa PIC, Augustino Vulu wametoa
pongezi hizo Aprili 1, 2023 baada kutembelea mradi huo wa kusambaza Umeme
Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (R3R2) ambao umeonesha kuleta tija kwa
wananchi.
Vulu alisema Serikali imetenga zaidi ya Sh. bilioni 50 kwa ajili ya
kukamilisha miradi minne inayotekelezwa mkoani humo miradi ambayo ikikamilika
itakuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa wananchi.
“Leo tupo hapa Shule ya Sekondari ya Irisya ambapo tumeshuhudia jinsi
wanafunzi na wananchi wanaoishi katika kijiji hicho jinsi walivyoanza kunufaika
baada ya kupata umeme ambao umewekwa kwenye madarasa na wanafunzi kuanza kujisomea
hadi usiku.” alisema Vulu.
Vulu alisema wanatarajia kuona ufaulu ukiongezeka kwa wanafunzi wanaochukua
masomo ya sayansi kwani hivi sasa watakuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo baada
ya kupata umeme.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REA), Janet Mbene alisema mradi huo
umeanza kuleta faida katika Shule ya Sekondari ya Irisya na vijiji hivyo vitatu
vinavyopakana na shule hiyo na lengo likiwa nikuona umeme huo unawasaidia,
kiuchumi, maendeleo kwa maana ya elimu na mambo mengine.
“Kuletwa umeme katika vijiji hivi sisi kwetu ni furaha na tunajua sasa
tumetimiza wajibu wetu kuhakikisha kuwa yale malengo tuliojiwekea yanatimia”
alisema Ndeme.
Ndeme aliwataka wananchi kuitumia fursa hiyo ya kuwekewa umeme kwa
kujiunganisha kwenye maeneo yao ya makazi na biashara na wabuni biashara ambazo
zinatumia umeme kwa ajili ya kujinufaisha kwa kuleta maendeleo ya mtu mmoja
mmoja, vijiji, wilaya nzima na mkoa kwa ujumla.
Aidha Ndeme amewaomba wananchi wa maeneo hayo yaliyopata umeme kuongeza
tija ya uzalishaji wa mazao wanayolima kwa kuyachakata na kuyaongezea thamani
na kujikuta wakikua kiuchumi.
Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini
mkoani Singida kwa Kamati, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy
ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala hiyo imetoa jumla ya shilingi bilioni
73.1 na Dola za Marekani 988,707.60 ili kuhakikisha miradi minne inayotekelezwa
mkoani humo inakamilika na wananchi wanapatiwa huduma ya nishati hiyo ili
kujipatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha, ameeleza zaidi kuwa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa
Pili katika Wilaya za Ikungi na Singida unatekelezwa na Mkandarasi M/s Central
Electricals International Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 26.3 na katika
Wilaya za Iramba, Manyoni na Mkalama, unatekelezwa na M/s CRJE – CTCE
Consortium kwa gharama ya shilingi bilioni 31.6
Amesema kuwa, maendeleo ya Mradi kwa wastani yamefikia asilimia 70.21
ambapo kwa Wilaya za Ikungi na Singida, Mkandarasi amefikia asilimia 77.54 na
Wilaya za Iramba, Manyoni na Mkalama, Mkandarasi amefikia asilimia 62.87.
Mkoa wa Singida una jumla ya vijiji 441 ambapo vijiji 287 vimekwishapatiwa
umeme kupitia miradi ya umeme vijijini iliyotekelezwa awali. Vijiji 169
vilivyobaki vinaendelea.</p
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida, Mhandisi
Florence Mwakasege alisema shirika hilo limekuwa likishirikiana na REA katika
kazi hiyo ya kutoa huduma kwa wananchi na ndio maana ilipo REA na TANESCO ipo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REA), Janet Mbene, akizungumzia manufaa ya mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akizungumza kwenye ziara hiyo.
|
Ltd akijitambulisha pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo.