Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Ndugu, Daudi Yasin amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC).
Huo ni mwendelezo wa ziara yake katika kukutana na makundi mbalimbali ndani ya mkoa wa Iringa kwa lengo la kukiimarisha chama hicho ndani ya Mkoa wa Iringa.
Mazungumzo baina yake na viongozi hao wa IPC, yaliyo fanyika leo Aprili 1, 2023 kwa takriban masaa mawili yalilenga kuimarisha mahusiano baina ya wanahabari na CCM.
“Ukiniuliza ajenda yangu leo ni moja tu kujenga uhusiano baina yetu, tushirikiane Kuijenga CCM,” amesema Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Iringa, Bw. Yasini.
Viongozi wa IPC walimpongeza Mwenyekiti Yasin kwa mkakati wake wa kukutana na makundi mbalimbali na kuahidi ushirikiano kwenye kazi za chama hicho.
Pia viongozi hao wa IPC
walitoa maoni na ushauri katika masuala mbalimbali ambapo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa
Ameahidi kufanyia kazi maoni na ushauri huo wa viongozi wa IPC.