**************************
NA EMMANUEL MBATILO
Chama cha Waajiri nchini Tanzania (ATE) kimesema bado kuna haja ya kuboresha na kurekebisha sheria za kazi ili kuweza kuendana na hali ya sasa kwani baadhi ya sheria za kazi na utekelezaji wake zinahitajika kuboreshwa Zaidi ili kutatuta changamoto hizo.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam na waandishi wa habari juu ya wiki ya huduma kwa wateja Mkurugenzi mtendaji wa ATE, Dkt, Aggrey Mlimuka amesema kuwa kuna haja ya sheria kurebishwa katika maeneo kadhaa ikiwemo masaa ya kazi,fidia za mfanyakazi anapoachishwa kazi,namna ya kupunguza wafanyakazi pamoja na mambo yote ambayo kwa sasa yanaonekana kuwa na changamoto ili kuweza kuboresha sheria vizuri na kuweza kutoa haki sawa kwa mwajiri na mfanyakazi.
Aidha amesema kuwa wameanzisha rasimi utaratibu wa kila wiki kutoa taarifa muhimu kuhusu masuala ya sheria za kazi na mahusiano sehemu za kazi ikiwa lengo ni kuwaelimisha waajiri kuhusiana na sheria za kazi pia kuepuka migogoro ya mara kwa mara kwenye maeneo ya kazi na kujenga mahusiano sehemu za kazi mambo amabyo yanaleta tija na kuongeza uzalishaji na hatimaye kukuza ustawi wa uchumi wa nchi.
Akizungumzia juu ya wiki ya huduma kwa wateja kimataifa Dkt Mlimuka amesema kuwa ATE, wameamua kuanzisha wiki ya huduma kwa wanachama ili kuwapatia fursa wanachama kutoka sekta mbalimbali ya kuwapatia mrejesho kuhusu huduma zote wanazozitoa.