Na WAF- Lindi.
Naibu waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel leo amefanya ziara katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi, Sokoine na kuzungumza na watumishi pamoja na kusikiliza kero zao.
Dkt. Mollel pia amebaini uagizaji wa dawa (maoteo) ambao hauendani na mahitaji halisi, hali inayopelekea changamoto katika upatikanaji wa dawa.
“Ulivyoambiwa fanya maotea kwa mwaka mzima ukaandika 50,lakini mpka sasa mwaka haujaisha umeshaomba 16,000 na MSD wamekupa 2000, umetoa wapi hiyo data.” Amesema.
Aidha, Dkt.Godwin Mollel amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii ili kufikia lengo la rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan la kutaka wananchi kupata huduma bora za afya kwa kila mwananchi.