Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Menejimenti ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kujitambulisha na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Menejimenti ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kujitambulisha na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kujitambulisha na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kujitambulisha na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI Dar es Salaa
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti ya Watumishi Housing Investments (WHI) akiwa kwenye ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
…………………………………….
Na. Mary Mwakapenda-Dar es Salaam
Tarehe 29 Machi, 2023
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameielekeza Menejimenti ya
Watumishi Housing Investments (WHI) kujenga nyumba za watumishi
kwenye maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kuishi ili
kuwawezesha watumishi wote hata walio kwenye maeneo ya
pembezoni kupata makazi bora ya kuishi yatakayowawezesha
kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo leo wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kujitambulisha na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa
Watumishi Housing Investments jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kikwete amesema pamoja na kazi nzuri iliyofanywa na
inayoendelea kufanywa na Watumishi Housing Investments, ni vizuri
zaidi wakafikiria kujenga nyumba nyingi zaidi maeneo yenye uhitaji
mkubwa wa nyumba hizo, akitolea mfano wa maeneo ya pembezoni
mwa nchi ambayo ndio yenye uhitaji mkubwa wa nyumba.
“Mnafanya kazi nzuri sana ya ujenzi wa nyumba hizi, lakini mnatakiwa
kuangalia fursa, maeneo gani yana uhitaji mkubwa wa nyumba, hasa
maeneo ya pembezoni ili hata wanaohamishiwa huko wafurahie maisha
na kutekeleza kikamilifu jukumu la kutoa huduma bora kwa wananchi,”
Mhe. Kikwete amesisitiza.
Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, pamoja na haki na stahiki nyingine
wanazopata watumishi, mazingira mazuri ya kuishi ni jambo lingine la
msingi ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na WHI wakati wa
utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi watumishi wa
umma.
Mhe. Kikwete amesema ni matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona watumishi wa
umma wanafanya kazi kwa bidii na maarifa, hivyo katika kufikia malengo
ya Mhe. Rais, Watumishi Housing Investments wana nafasi kubwa ya
kuunga mkono lengo hilo la Mheshimiwa Rais kwa kujenga nyumba
bora kwa ajili ya kuziuza na kuwapangisha watumishi wa umma nchini.
“Taasisi zinazojenga nyumba ziko nyingi, wengine wanajikita kwenye
ujenzi wa nyumba kwa ajili ya mwananchi yeyote lakini sisi Watumishi
2
Housing Investments tuna malengo yetu ambayo yamejikita kwa
watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, hivyo
tunapaswa kuhakikisha malengo ya taasisi yanatimia.
Mhe. Kikwete ameisisitiza Menejimenti ya taasisi hiyo kutosita
kuwashirikisha Viongozi na Menejimenti ya Ofisi ya Rais, menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora pale wanapokutana na
changamoto au kama kuna mwongozo wowote wanaouhitaji katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, Mhe. Kikwete ameitaka taasisi hiyo kutangaza utekelezaji wa
majukumu ya taasisi yao ili yafahamike kwa wahusika.
“Watumishi wanahitaji kuyajua majukumu yenu, mjitahidi kujitangaza ili
kuwafikia kiurahisi tunaowalenga na kuifanya taasisi yetu kuwa kimbilio
la watumishi pale wanapohitaji kuwa na nyumba iwe ya kununua au
kupangisha,” Mhe. Kikwete amefafanua.
Mhe. Kikwete amehitimisha ziara yake ya kikazi ya kuhimizia uwajibikaji
kwa watumishi wa taasisi za umma zilizo chini ya Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora jijini Dar es Salaam.