Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua jengo la Benki ya NBC mjini Bariadi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 25, 2023. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano, Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sami wakikata utepe wakati Waziri Mkuu alipozindua jengo la Benki ya NBC mjini Bariadi, Machi 25, 2023. Wa nne kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Bariadi, Mhandishi Kundo Mathew, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda, kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange na wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua jengo la Benki ya NBC mjini Bariadi, Machi 25, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi kuhusu huduma zitakazotolewa katika Benki ya NBC baada ya kuzindua jengo la benki hiyo mjini Bariadi Machi 25, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi baada ya kuzindua jengo la benki hiyo mjini Bariadi mkoani Simiyu, Machi 25, 2025. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Benki ya NBC baada ya kuzindua jengo la Benki hiyo mjini Bariadi mkoani Simiyu, Machi 25, 2023. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)