Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula
akiwasilisha Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake kwa mwaka wa
fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi wakifuatilia kwa makini kuhusu uwasilishaji wa Makadirio ya Matumizi na
Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi wakifuatilia kwa makini kuhusu uwasilishaji wa Makadirio ya Matumizi na
Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
Baadhi ya Wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili
na Utalii wakimfuatilia kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt.Angeline Mabula wakati akiwasilisha kwao Makadirio ya Matumizi na
Mapato ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24
…………………………………..
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ameimbia
kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kuwa Wizara yake inakuja na
mageuzi makubwa ya tehama kwa lengo la kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi ya
pango la ardhi ili serikali iweze kuongeza mapato yake kupitia kodi hiyo.
" Tunaenda kuwa na mageuzi makubwa kwa upande wa tehama kwa kuwa Wizara
sasa inapitia mifumo upya ili wananchi waweze kupata ujumbe kwa njia Simu kama njia
rafiki ya ukusanyaji mapato."Alisema Dkt.Angeline Mabula Waziri Wizara ya Ardhi.
Waziri Mabula amesema hayo leo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii inayokutana leo kujadiliana kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa mwaka
wa fedha 2022/2023 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa
mwaka wa fedha 2023/24.
Waziri Mabula ameiambia kamati hiyo kuwa hata kabla ya bunge la bajeti kuanza
baadhi ya wananchi wataanza kupokea ujumbe mfupi kupitia mitandao ya simu kuhusu
makadirio ya kodi ya pango la Ardhi.
Waziri Mabula aliongeza kuwa zoezi hili liko mbioni kukamilika kwani timu ya wataalamu
wa tehama iko kazini na wananchi wataanza kulipia kama zilivyo bili za maji
zinazotolewa na mamulaka za maji hapa Nchini.
Akiwasilisha taarifa yake kwa Wabunge hao Waziri Mabula amesema azima ya serikali
ni kuimarisha usalama wa milki kwa kuhakikisha kila kipande cha Ardhi nchini
kinatambuliwa,kupimwa na kumilikishwa na hivyo kudhibiti Migogoro ya matumizi ya
Ardhi.
Waziri Mabula aliongeza kuwa hatua hiyo itawezesha kukua kwa uchumi wa
mwananchi mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.
Aidha Waziri Mabula ameiambia kamati hiyo kuwa Wizara yake imeendelea kufanyia
kazi mapendekezo na ushauri vilivyotolewa wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi
jijini Arusha na kuwapongeza kamati kwa jinsi ushauri wao unavyo unavyowezesha
kufikia malengo ya Serikali.
Waziri Mabula amewasilisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi fungu 48 na Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi
fungu 3 kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambayo yanajumuhisha Taarifa ya Utekelezaji
wa Bajeti kwa mwaka 2022/23 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa
mwaka 2023.