Mhandisi wa Tanga Uwasa Salum Ngumbi wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akizungumza wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.
Na Oscar Assenga,TANGA.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi Mazingira (Tanga Uwasa) umeweka bayana mikakati waliokuwa nayo kwa sasa wa kufufua visima vyote vya maji zilivyokuwa vinatumika ili kupunguza kero ambazo zinaweza kuzuilika.
Mkakati huo uliwekwa hadharani na Mhandisi wa Tanga Uwasa Salum Ngumbi wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.
Alisema visima hivyo vipo katika maeneo ya uwanja wa ndege,na Mwakileo ikiwa ni mbadala wa maji kwa wananchi,ikitokea kupungua kwa maji ili waweze kuvitumia kwa ajili ya kuwafikia wananchi pasipo kuwepo na kizuizi chochote.
Alisema pamoja na kufufua visima hivyo lazima watahakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambao wamekuwa wakiwahudumia kila siku ili kuondosha vikwazo ambavyo wanaweza kukutana navyo.
“Mpango tulionao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata maji kukidhi mahitaji muhimu kwa wananchi,pia tuna mpango wa kuanza miradi ya maendeleo katika mamlaka ya maji ikiwemo mradi wa ujenzi wa kutanua bwawa la mabayani na tunatarajia uanze septemba mwaka huu”.
Upatikanaji wa maji kwa siku katika maeneo yote ni lita 30,000,ambapo kwa sasa mtambo uliopo ni kwa ajili ya kutanua uzalishaji kufikia lita 45,000 ambayo itasaidia kukidhi haja kwa wananchi wote.
“Kwa sasa upo mradi uliogharimu zaidi ya sh.Bilioni 10 ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji katika jamii kwani tunafanya hivi kuhakikisha yaliyojitokeza kwa wananchi kukumbana na changamoto ya huduma hii hayajitokezi tena na hali iliweza kuwaathiri wakazi katika maeneo mbalimbali Jijini Tanga kutokana na mvua kutokunyesha kwa kipindi kirefu na kusababisha Bwawa la Maji kupungua”Alisema
“Tuna mitambo minne ambayo miwili ndio inatumika Kwa Sasa ns inasaidia kupandisha Maji mpaka kuwafikia wananchi na mingine miliwi ipo kwa ajili ya akiba kama ikitokea mmoja kati ya hii ikiharibika”
Mhandisi salum aliwashauri pia wakazi wa Tanga kupanda miti itakayosaidia kutunza mazingira muda wote na kusababisha kunyesha mvua za mara Kwa mara Ili kuwepo na upatikanaji wa Maji
“Suala la miti kuwa michache katika maeneo yetu tunayoishi ni Changamoto niwaombe wananchi kupanda miti Ili kusaidia mazingira yetu muimarika na Hata mvua ziweze kunyesha Ili tupate maji muda wote”Alisema
Akielezea changamoto ya ukosefu wa Maji tokea mwezi Novemba Mwaka jana ambapo alieleza mpaka kufikia mwezi Machi mwaka huu hali hiyo imeweza kuimarika hivyo amewaomba wakazi wote kutumia Maji kwa umakini na ikiwemo kujenga utamaduni ya kuyahifadhi kwa ajili ya kuwasaidia katika maatumizi yao.
“Kuanzia machi Mwaka huu hali ya upatikanaji wa Maji imeanza kuwa shwari ingawaje haijafikia asilimia 100 , maeneo mengi yanapata maji na vilevile Tanga Uwasa tumejipanga kutatua changamoto iliyokuwepo”Alisema Mhandisi Salum
Naye kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara kutokea kwenye mtambo wa kutibu Maji wa Mowe Amos Rwehangana alisema kwa sasa hali ya kutoka kwa Maji ipo vizuri katika maeneo mbalimbali yakiwa masafi na hayawezi kuleta athari yoyote katika jamii na hiyo inatokana na juhudi walizonazo .