Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa Kikao cha kupokea na kujadili taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, kikao kilichofanyika leo Machi 12, 2023 katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Mhe. Florent Kyombo akizungumza wakati wa kikao cha kupokea na kujadili taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, kikao kilichofanyika leo Machi 12, 2023 katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi wakiwa katika Kikao cha kupokea na kujadili taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kikao kilichofanyika leo Machi 12, 2023 katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga katika viwanja vya Bunge mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha kupokea na kujadili taarifa kuhusu muundo na majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kikao kilichofanyika leo Machi 12, 2023 katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
………………………………………
Ofisi ya Makamu wa Rais imewasilisha Taarifa kuhusu muundo na majukumu yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha taarifa hiyo ambayo pia imejadiliwa na Kamati hiyo ya Bunge kwa upande wa Muungano.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mhe. Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kuhusu Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo kwa upande wa Zanzibar.
Amesema ipo haja ya kutoa elimu hiyo kwa viongozi wa mabaraza ya wilaya ili wapate uelewa kuhusu usimamizi wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya majimbo yaliyopo Zanzibar.
Akiendelea kuzungumza wakati wa kikao hicho, Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha wananchi wa pande zote mbili za Muungano wanafaidika na rasilimali zilizopo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Maji na Mazingira Mhe. Mhe. Florent Kyombo ametaka ushauri uliotolewa na wabunge uzingatie.
Wakichangia taarifa hiyo baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakiwemo Mhe. Rashid Shangazi, Mhe. Tumaini Magesa na Mhe. Edward Olelekaita wameshauri iongezwe nguvu katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Wabunge hao pia wameshauri Ofisi ya Makamu wa Rais iendelee kufanya kazi kwa karibu na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na kufuatilia kwa karibu wa miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Dodoma kwani baadhi ya miti inakufa.