Balozi Mwanaidi Maajar, Makamu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO akizunguma katika kongamano la wanawake wa TANESCO lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya wanawake duniano inayoadhimishwa machi 8, kila mwaka duniani kote.
……………………………….
Shirika la Umeme Nchini Tanzania -TANESCO limewataka wanawake nchini kutumia juhudi katika ufanyaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa Leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania- TANESCO Balozi Mwanaidi Maajal wakati akizungumza katika Kongamano la wanawake wa Shirika Hilo ikiwa ni katika kusheherekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambalo limefanyika Kwenye Ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam.
Balozi Mwanaidi amesema kuwa tar nane Machi ni siku muhimu kwa wanawake kwani huwaleta pamoja na kujadili Masuala mbalimbali yakiwemo mafanikio yakuleta usawa wa kijinsia kwenye nafasi za maamuzi kuhusu Maisha yao.
“Siku hii ya wanawake pia tunasheherekea mafanikio yetu kwa kupongezana kwani kauli Mbiu ni muafaka kwa kuwahamasisha wanawake kuchangamkia fursa za kibiashara na ubunifu wa Teknolojia ambazo wanawake pia hawajabaki nyuma”amesema Balozi Mwanaidi
Amewashauri wanawake wa TANESCO kuendelea kuonyesha ubunifu katika shughuli zao bila kujali nafasi zao wanazotumikia kwani kufanya hivyo itawaongezea kupata kipaumbele katika kazi zao.
Aidha amesema wataweka utaratibu wa Kimfumo kuhakikisha idadi ya wanawake katika Shirika la TANESCO Ili waweze kuonyesha ujuzi wao kupitia nafasi mbalimbali ndani ya shirika hilo.
Katika hatua nyingine Balozi Mwanaidi amewapongeza wafanyakazi wa TANESCO Kwa kutumia siku ya wanawake kupanda miti nchi nzima jambo ambalo linasaidia kuyatunza Mazingira.
“Zoezi ambalo mumelifanya kwa kupanda litasaidia kuiamsha na kuielimisha jamii kuzingatia utunzaji wa mazingira Ili kulinda vyanzo vya ambavyo Shirika ni maeneo tegemezi katika shughuli za uzalishaji wa Umeme”ameendelea kusisitiza Balozi Mwanaidi
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2023, ” Ubunifu na mabadiliko ya Teknolojia, chachu katika kuleta usawa wa kijinsia”Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka kuanzia Machi 1 na kufikia kilele Machi 8 ambapo kwa mwaka huu yamefanyika kila mkoa yakiratibiwa kupitia ofisi ya wakuu wa mikoa na halmashauri zote nchini.
Dkt. Elly Waminiel mtaalamu wa falsafa na saikolojia akitoa mada katika kongamano hilo lililfanyika janakwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Irene Kawili kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA akitoa mada katika kongamano hilo la wanawake wa TANESCO.
Afande Lea mbunda, mkuu wa Dawati la jinsia na watoto polisi Kanda Maalum akiwasilisha mada katika kongamanohilola wanawae wa TANESCO.
Elihuruma Ngowi Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa wadau TANESCO akishiriki katika kongamano hilo la wanawake TANESCO.
Irene Marobe Kaimu Meneja Masoko na shughuli za chapa TANESCO akitambulisha baadhi ya wageni na viongozi wa TANESCO ktika kongamano hilo.
Neema Mbuja Afisa Uhusiano Mwandamizi TANESCO akitoa ratiba ya kongamano hilo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere.
Balozi Mwanaidi Maajar, Makamu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO akiwasili katika kongamano la wanawake wa TANESCO lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya wanawake duniano inayoadhimishwa machi 8, kila mwaka duniani kote.
Picha mbalimbali zikionesha wanawake wafayakazzi wa TANESCO wkiwa katika kongamano hilo.
Balozi Mwanaidi Maajar, Makamu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO na mjumbe wa bodi hiyo CPA Zawadia Nanyaro wakiserebuka na muziki wa mwanamuziki Christian Bella.
Mwanamuzziki Christian Bella akitumbuiza katika kongamano hilola wanawake wa TANESCO.
Neema Mbuja Afisa Uhusiano Mwandamizi TANESCO kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Gea Habib Mtangazaji wa Clouds Media na MC wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Balozi Mwanaidi Maajar na kamati ya maandalizi ya Kongaman hilo.
Picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Balozi Mwanaidi Maajar na wanawake wapambanaji wa TANESCO katika kongamano hilo.