Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA Dkt. Ladislaus Chang’a akifungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu utabiri wa Hali ya hewa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Kibaha Conference Center mjini Kibaha mkoani Pwani Leo.
Mwandishi wa habari kilutoka Kituo Cha luninga Cha Channel Ten Bi. Dorcas Mtenga akitoa mchango wake Katika semina hiyo.
Mwandishi wa habari Bernald Lugongo Kutoka magazeti ya serikali TSN akiuliza swali wakati mada mbalimbali zikiendelea Katika semina hiyo.
Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano TMA Bi. Monica Mutoni akifafanua jambo Kwa waandishi wa habari Katika semina hiyo iliyofanyika Leo mjini Kibaha.
Mmoja wa wataalam wa kuchakata utabiri wa Hali ya hewa Kutoka TMA akielekea namna kazi ya kuchakata taarifa hizo za utabiri inavyofanyika.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania -TMA imeendelea kuwasisitiza wanahabari kuwa mabalozi wa kuwafahamisha watanzania umuhimu wa kuzifuatilia taarifa mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka hiyo ili kuweza kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza yanayosababisha na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yameelezwa Leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania -TMA Dkt. Ladislaus Chang’a WAKATI akifungua Warsha ya wanahabari mjini Kibaha Mkoani Pwani kuhusu muelekeo wa msimu wa Masika kuanzia Mwezi Machi hadi Mei Mwaka huu sambamba na kuwajengea uwezo namna ya kuandika na kuripoti taarifa za Hali ya Hewa.
Mkurugenzi Huyo amesema Warsha hiyo ni muendelezo wa juhudi za kuhakikisha taarifa mbalimbali zinawafikiwa watanzania na wanahabari kuendelea kuwa nguzo muhimu katika kuihabarisha Jamii.
“Dunia yetu na nchi yetu inakabiliwa na ya Hali ya hewa hivyo jamii inavyopata uelewa itafahamu namna ya kukabiliana na changamoto hizo ambazo zimekuwa zikijitokeza katika maeneo mbalimbali”amesema Chang’a
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka kuendelea kuwa Mabalozi Wazuri kwa kuendelea kusisitiza jamii kufahamu umuhimu wa taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Ili waweze kupata uelewa wa kuhusu Hali mbaya ya Hewa.
Kuhusu mafanikio ya Utabiri Chang’a amesema kwa kipindi hiki Mamlaka imekuwa ikifanya Utabiri Kwa maeneo madogomadogo katika Wilaya mbalimbali hasa kwa yake yanayopata msimu mmoja wa mvua.
“Kazi munayoifanya ni Muhimu sana katika Jamii hivyo tunaomba iendelee Ili kutoa elimu kwa Jamii ifahamu kuwa wenye Mamlaka ya kutoa taarifa zote zinazohusiana na Hali ya Hewa”ameendelea kusema Dkt Chang’a
Amesisitiza kuwa Warsha hiyo ni ya kipekee kwani Afrika TMA kwani ndo imekuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wanahabari kuhusu kupata uelewa wa Masuala ya Hali ya Hali ya Hewa.