Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Daniel Chongolo amesema imefika wakati Serikali iangalie namna ya Kuongeza Bajeti yake kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwani ni wazi wakala huo kwa sasa matokeo yake yameonekana na bado bajeti ni ndogo kulingana na ukubwa wa urefu wa Barabara za Vijijini na Mijini.
Chongolo ameyasema hayo leo Katika hafla ya makabidhiano ya Magari 54 kwa TARURA kwa ajili ya mameneja wa mikoa pamoja na Pikipiki 916 iliyofanyika leo Jumanne 14/2/2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji ulioko eneo la mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya watendaji wa kata kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ikiwa na lengo la kuwarahisishia watendaji wa kata kuwafikia wananchi na kufikia walengwa kwa wakati ambapo mgeni rasmi katika Hafla hiyo alikua ni Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Philip Isdor Mpango.
“Mhe.Makamu wa Rais naomba niseme,TARURA kwa sasa imekuwa na kazi kubwa na kazi inayofanyika inaonekana hivyo nashauri Serikali ione namna ya kuongeza bajeti kwa wakala huu kwani mtandao wa barabara za vijijini bado unahitaji katengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hasa wakulima ili waweze kusafirisha mazao yao hasa baada ya mavuno na serikali ikiliangalia hilo naamini tutakuwa tumeweza kupiga hatua hasa kwa kupunguza au kumaliza kabisa Changamoto ya kero ya barabara,” Amesema Chongolo
Amemuambia Mhe Makamu wa Rais Kwa kusema “Nishauri tu kwa waziri wa TAMISEMI kwa kuwa lengo kuu la kugawa vitendeakazi hivi hasa Pikipiki zinazokabidhiwa kwa watendaji wa kata ambazo tu moja ni zaidi ya 900 ni vyema zikawekewa utaratibu mzuri wa kuzitunza ikiwa ni kuanzia kuziweka Mafuta pamoja na Matengenezo iwe kwa mkurugenzi wa Jiji,Manispaa,Mji au halmashauri kwani zitakuwa katika uhakika wa matumizi hasa tukizingatia pikipiki hizi ni mali ya umma na lengo lake ni kuhudumia wananchi
Amemalizia Katibu mkuu huyo wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.