Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Jukwaa hilo Ndugu Deodatus Balile amesema wanamshukuru Rais Samia kwa kuonyesha ushirikiano kusikiliza na kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zinavikabili vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa baadhi vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa pamoja na kupunguza gharama za leseni za Luninga kutoka milion sabini na tatu kwa mwaka hadi milion 32 kwa mwaka.
Tuliwasilisha Agenda kumi na nne Ikulu kwa Mheshimiwa Rais na tunamshukuru mheshimiwa Rais kwani kati ya hizo agenda nyingi za kikanuni zimesharekebishwa lakini pia leo bunge lilipoisha tumeona mswada umesomwa na bunge limerejeshwa na litaonenywa mubashara kupitia vyombo vya habari
Amesema
Deodatus Balile’.
Aidha Balile amemshukuru Waziri wa Habari Mawasiliano na technolojia ya habari Nnape Nnauye kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa kwa Jukwaa hilo kwani kuna baadhi ya changamoto nyingi walizokuwa wakikutana nazo katika zoezi zima kutafuta haki na uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni kuhakikisha kwamba yale yaliyokuwa magumu yaliweza kuwekwa katika usawa.
Ameongeza kwamba anamshukuru pia mwanasheria Mkuu wa Serikali kwani ameonyesha ushirikiano mkubwa na kuonyesha kwamba anapenda nchi hii iwe na sheria ambazo zina uhuru wa habari.
Baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza mswada wa marekebisho ya sheria ndogo ndogo tunaamini wataweka kwenye website ya Bunge tutaisoma na pamoja tutaanza kuijadili tutaona kama yaliyomwo yatatusaidia kujenga Taifa lililo moja na kwamba kila mwanachi maoni yake yataheshimika na kusikilizwa?
Sisi Jukwaa la wahariri tunapigania uhuru wa vyombo vya habari lakini sio kwa ajili ya waandishi wa habari tu ni kwa ajili ya wananchi wote kwani kila mwanachi ana haki ya kupata habari pamoja na haki ya kujieleza, na huu ndio utakuwa mwanzo wa Demokrasia nchini, ukuaji wa utoaji mawazo, ukuaji wa nchi yetu, ustaarabu katika nchi yetu na tutakuwa na utawala bora na utawala wa sheria.
Amesema Balile.
Kwa upande wake mjumbe wa Jukwaa hilo ndugu Said Salim amesema kwamba wanachokifanya TEF ni kile wanachokidai haki ya kujieleza Watanzania wawe watu wenye uhuru wa kujieleza, kusikia sauti za wananchi tofauti wakitoa maoni yao ndio utawala bora.
Naye Angella akilimani kwa niaba ya kamati ya utendaji amesema anaungana na Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri na waandishi wote kuishukuru Serikali kwa Mswada huo kusomwa bungeni kwa mara ya kwanza na ana Imani kwamba anategemea kuona sheria kandamizi sasa zitaondolewa na utakuwepo uhuru wa vyombo vya habari na maisha bora kwa waandishi habari