Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini SACP Ramadhani Ng’anzi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuelekea kufanyika kwa ukaguzi wa magari ambao unaanza Leo mpaka Mwezi wa tatu.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini SACP Ramadhani Ng’anzi akionyesha njia mbalimbali watakazotumia katika kufanya ukaguzi wa magari.
……………………….
NA MUSSA KHALID
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini SACP Ramadhani Ng’anzi amewaagiza wakuu wa usalama barabarani kutenga maeneo maalum ya kufanya ukaguzi wa magari ili viweze kuwa na usalama vinavyokuwa barabarani.
Pia Kamanda Ng’anzi amesema zoezi hilo la ukaguzi wa magari linaanza kuanzia leo Feb 6 ni kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani kifungu cha 39 kuanzia kifungu kidogo cha kwanza mpaka cha kumi na sita.
Hayo ameyaeleza wakati akizungumza jijini Dar es salaam ambapo amesema lengo la zoezi hilo ni kupima umadhubuti wa magari kwa vigezo vyote ikiwemo mifumo mbalimbali kuanzia breki.
‘Naagiza kuanzia leo RTO wote mutenge maeneo maelum na tunatoa kipindi kuanzia tarehe ya leo Feb 6 mpaka tar 13 mwezi Machi mwaka huu tutakapo fanya sherehe za wiki ya nenda kwa usalama barabarani’amesema Kamanda Ng’anzi
Amesema matarajio yao ni kwamba madereva wote wamagari yanayobeba abiria,mizigo,mafuta,magari ya wanafunzi,pikipiki na bajaji yote hayo yanapaswa kufika katika vituo vya polisi ili kuweza kufanyiwa ukaguzi maalum na Jeshi hilo litatoa hati maalum ili kuwa na vigezo vya kukaa barabarani.
Aidha kuhusu usalama wa barabara Kamanda Ng’anzi amesema kabla ya tukio la juzi la ajali zilikuwa ni salama hivyo wanaendelea na uchunguzi wa ajali hivyo amewasisitiza madereva kuendelea kuwa makini wawapo barabarani.
‘Kutokana na tukio la ajali lililotokea katika Mkoa wa Tanga sasa hivi tumekaa na tunafikiria kutengeneza kanuni vilevile ya kudhibiti magari ya mizigo yanayotembea usiku kwa sababu tumeona ajali nyingi zinaztokea usiku wakati wa kuovatek na wakati huo pengine askari unakuta wamejipumzisha au majukumu mengine hivyo tutakuja na mkakati madhubuti’ameendelea kusema Kamanda Ng’anzi
Katika hatua nyingine Kamanda Ng’azi ametoa wito kwa wananchi wote kuepukana na vitendo vya kwenda kufanya wizi katika maeneo amabyo ajali imetokea kwani kufanya hivyo pindi wakibainika watachukuliwa hatua kali.