Happy Bigala Festo mama wa watoto wanne mkazi wa kijiji cha Matuga wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani amelazikika kuhamia kwenye banda la bata na kuku pamoja na watoto wake wanne huku wananchi wenzake pia wakihangaika huku na kule wasijue la kufanya, baada ya kuvunjiwa nyumba na watu wasiojulikana wanaodaiwa kutumwa na mwekezaji na kuvunja nyumba zaidi ya 92 katika kijiji hicho na vitongoji vya jirani mwishoni mwa wiki iliyopita.
Happy ameyasema hayo wakati akizunguma na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo mara baada ya kupata taarifa za wananchi kuvunjiwa nyumba ikidaiwa eneo hilo ni la mwekezaji ambaye wananchi hao wamedai hawamjui.
Happy amesema alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo baada ya dada yake kumpatia eneo ili aishi na watoto kulingana na ugumu wa maisha huku akieleza kuwa kwa sasa wanaishi kwenye banda la kuku na bata na chakula ni shida kwa sababu hawawezi hata kwenda kutafuta chochote kwakuwa vyakula na maliza zao vimeharibiwa katika bomoabomoa hiyo.
Happy pamoja na wanakijii wenzake wakizungumza katika nyakati tofauti wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia mgogoro wa kubomolewa nyumba zao pasipokuwa na taarifa kwa sababu hatua hiyo inawaacha wakiwa masikini huku watoto wakihangaika bila msaada wowote.
Wakizungumza zaidi wananchi hao wamesema kuwa ubomoaji huo umefanyika ghafla bila ya wao kupewa ya taarifa sababu nyumba zao pamoja na mali zao zimeharibiwa.
Naye mkazi wa eneo hilo Veronika Wilbati Chongolo amesema ameshuhudia nyumba yake ikivunjwa na kuibiwa vitu vyake huku Mwenyekiti wa serikali ya Kitongoji cha Matuga Geofrey Kazinduki akieleza kuwa ameshangazwa mpaka ofisi ya Mkurugenzi kutofahamu kuhusiana na zoezi hilo.
“Nilipofika eneo la tukio nikaonana na Mkuu wa askari aliyekuwa akisimamia zoezi hilo anaitwa Kadogosa, nikajitambulisha na kumuuliza kwa nini wanabomoa, akasema wao wanafuata amri waliyopewa kuvunja akanitaka niondoke haraka la sivyo watanishughulikia.”amesema Mwenyekiti
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kawawa Alfred Daniel Malega amesema hadi zoezi la uvunjaji linafanyika hakuwa na taarifa hizo na kudai kuwa zoezi hilo limemsikitisha na limefanyika kihuni.
Amesema alipowasiliana na RPC wa Pwani amemueleza kuwa yeye anazo taarifa juu ya kinachoendelea, lakini akamjulisha Wananchi hawajui mgogoro wa kesi unavyoendelea, pia akamweleza kilichofanyika si haki kwa kuwa bora Wananchi wangekuwa na taarifa wangejiandaa.
Amesema kuwa kwa mujibu wa Nyaraka ambazo zimeonekana za kesi hiyo zimeonesha kulikuwa na kesi kati ya Omari Kadri dhidi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Zegereni pamoja na Bartazar Simeon.
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Constantino Mwakamo amesema kuwa wakati alikuwa Mtendaji wa Kata ya Mlandizi ambapo eneo hilo ambalo limebomolewa ni moja ya maeneo ya kata husika,na hivyo hakuwahi kusikia kama kuna mgogoro katika eneo hili.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John akielezea kuhusu mgogoro huo amesema hiyo ni amri ya Mahakama,hivyo kama wahusika hawakubalini na hukumu wana haki ya kukata rufaa kwani Mahakama inahojiwa kwa mchakato wa kimahakama.
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Constantino Mwakamo akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Matuga ambapo amesema kuwa wakati alipokuwa Mtendaji wa Kata ya Mlandizi ambapo eneo hilo ambalo limebomolewa hakuwahi kusikia kama kuna mgogoro katika eneo hili.
Mwenyekiti wa serikali ya Kitongoji cha Matuga Geofrey akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu sakata hilo
Wkazi mbalimbali wa kitongoji hicho wakiwa wamepgwa na butwaa kufuatia bomoa bomoa hiyo.
Diwani wa Kata ya Kawawa Alfred Daniel Malega akifafanua zaidi kuhus tukio hilo baya kuwapata wananchi hao.
Mkazi wa eneo hilo Veronika Wilbati Chongolo ambaye amevinjiwa nyumba mbili na kanisa lake huku fedha za sadaka zikiibiwa akikusanya mabaki ya vifaa vya nyumba yake.
Happy Bigala Festo akiwa na watoto wake kwenye bandala kuku na bata ambalo wamehamia mara baada ya numba yao kuvunjwa.
Mmoja wa wazee wa kijiji hicho ambaye naye amevunjiwa nyumba yake akizungumza kwa uchungu huku machozi yakimbubujika.