Makamu wa Rais na Waziri wa Afya wa Zimbabwe Mheshimiwa Generali (Mstaafu) Constantino Chiwenga, Waziri viongozi kutoka mataifa mbalimbali wa Wizara za Afya wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Kidunia kwa Kanda ya Afrika wa kutokomeza Ukimwi kwa Watoto ifikapo mwaka 2030 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es salaam leo tarehe 1 Februari 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia wadau mbalimbali wa Afya kitaifa na kimataifa pamoja na Mawaziri wa Afya kutoka nchi 12 za Afrika ambazo ni Wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa kutokomeza Ukimwi kwa Watoto ifikapo mwaka 2030 kwa kanda ya Afrika wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Kidunia kwa Kanda ya Afrika wa kutokomeza Ukimwi kwa Watoto ifikapo mwaka 2030 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es salaam leo tarehe 1 Februari 2023.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza na wadau mbalimbali wa Afya katika mkutano wa kimataifa pamoja na Mawaziri wa Afya kutoka nchi 12 za Afrika ambazo ni Wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa kutokomeza Ukimwi kwa Watoto ifikapo mwaka 2030 kwa kanda ya Afrika wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Kidunia kwa Kanda ya Afrika wa kutokomeza Ukimwi kwa Watoto ifikapo mwaka 2030 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es salaam leo tarehe 1 Februari 2023.
Mwenyekiti wa Baraza la taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA). Bi. Leticia Kapela akizaungumza katika mkutano huo Kimataifa wa kutokomeza Ukimwi kwa Watoto ifikapo mwaka 2030 kwa kanda ya Afrika wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Kidunia kwa Kanda ya Afrika wa kutokomeza Ukimwi kwa Watoto ifikapo mwaka 2030 uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es salaam leo tarehe 1 Februari 2023.
WATAALAM wa Sekta ya Afya kutoka nchi 12 Barani Afrika pamoja na Mashirika ya Kimataifa ya kushughulikia masuala ya Ukimwi wamekutana kwa siku mbili kwenye kikao cha kupitia maazimio ya kutokomeza Ugonjwa wa Ukimwi fikapo 2030.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti Makamu wa Rais wa Zimbabwe Mhe. Costantino Chiwenga pamoja na Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu ambapo kimejadili mambo mbalimbali ikiwemokutokomeza maambukzi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ifikapo 2030
Nchi zinazotekeleza mkakati huu kwa Kanda ya Afrika ni pamoja na mwenyeji Tanzania, Cameroon, Code D’Ivore, DRC- Congo, Nigeria, Uganda, Zambia, Angola, Zimbabwe, Kenya, Afrika Kusini na Msumbiji ambazo ziliwakilishwa na mawaziri wa afya kutoka nchi hizo.
Akizungumza katika mkutao huo Mwenyekiti wa Baraza la taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA). Bi. Leticia Kapela amesema kuwa wanataka usalawa katika matibabu bila kubagua kundi lolote lile ili kila kundi lipate haki yake ya msingi.
Kapela alisema kuwa wanatoa rai hiyo kwa jamii kutoka na jamii kuendelea kuwanyanyapaa watu wenye VVU katika huduma mbalimbali za kijamii.
Alisema kuwa wapo tayari kushirikiana katika kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo 2030 kutokana na mkakati maalum uliowekwa na nchi hizo 12 za bara la Africa.
Kapela alisema kuwa wapo mstari wa mbele kuwafikia watu wenye VVU kufikia malengo ya 95,95,95 kwa lengo la kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa akina mama na watoto.