Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Dakar nchini Senegal tarehe 25-27 Januari, 2023 katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Januari, 2023.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na kuwaelezea Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Davos nchini Uswizi tarehe 16-20 Januari,2023 pamoja na Dakar nchini Senegal tarehe 25-27 Januari, 2023 katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Januari, 2023.
Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mkutano uliohusu Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Davos nchini Uswizi (tarehe 16-20 Januari,2023) pamoja na Dakar nchini Senegal tarehe 25-27 Januari, 2023. Mkutano huo wa Waandishi wa Habari umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Januari, 2023.
………………………………
Serikali imesema haitaondoa mfumuko wa bei za mazao kwa kumtia umaskini mkulima bali itachukua hatua kuhakikisha kuwa mlaji naye analindwa.
Pia imesema itahakikisha inaweka uwiano wa mazao ya chakula kwa kuingiza chakula sokoni kwani kama serikali huo ndio muelekeo watakaouchukua.
Hayo yameelezwa leo Ikulu jijini Dares Salaam na Waziri wa Kilimo Husein Bashe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Uswizi na Senegali.
‘Mazao ya wakulima ni mali yao wanahaki ya kuyauza popote na sisi serikali hatutazuia mkulima kuuza mazao yake popote kwani kwa muda mrefu wamekuwa maskini kwa manufaa ya watu wengine’amesema Waziri Bashe
Amesema kwa sasa uwezo wa kuhifadhi chakula umeongezeka kutoka tani laki 200.000 mpaka laki 500.000 hivyo wakati wa msimu wa kuvuna watanunua mahindi na mpunga kiasi cha kutosha ili kujiweka sawa kama kutatokea mazingira ya uhaba wa chakula.
Aidha Waziri Bashe amesema mipango ya serikali itahakikisha inanunua mazao ya mkulima kwa bei nzuri ili kuweza kumlinda mkulima kama anavyolindwa mlaji.
‘Chukuenti takwimu za toka mwaka 2018 mpaka leo angalieni ongezeko la bei za vyakula hasa mazao ya nafaka kumekuwa na tabia ya bei kupanda toka mwezi wa 10,11,12 mpaka wa tatu bei zinaanza kushuka kwa sababu tunaanza kuzalisha lakini mjadala wan nchi tusijadili bei tujadili tija ya mkulima’ameendelea kusema Waziri Bashe
Kuhusu sekta ya umwagiliaji Waziri Bashe amesema serikali imeamua kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa mara ya kwanza ili wasiweze kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Amesema kama nchi luma hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo na kilichotumika mpaka sasa ni hekta milioni 10 na haijafika hata asilimia 50 na eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta milioni 29 na zilizotumika ni asilimia 2.7 sawa na hekta 7,20,000 ndizo zimetumika , mwaka huu wa bajeti wameingia mkataba wa kujenga hekta 97000 ili kuingiza kwenye mtandao wa umwagiliaji
“Sasa hofu ya maeneo kuvamiwa ni kuwepo tu kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi, na Serikali imeamua sasa itakuwa inachukua maeneo ya mashamba(block farm) kisha tunaandaa na kusafisha na kuziweka na kugawa kwa vijana baada ya kupitia mchakato maalum ambao tumeuweka,”amesema Bashe.
Waziri Bashe ameongeza kuwa serikali inatambua changamoto ya ardhi na mitaji ambayo vijana wanakutana nayo, hivyo mpango wa Serikali imeamua kumaliza changamoto hizo kwani vijana watapewa ardhi na wakati huo huo Serikali imetenga fedha kupitia mfuko wa pembejeo na mwaka huu wameweka Sh.bilioni tatu.
“Mfano mpaka sasa wameshaomba karibu 16000 ambao wameomba kwa njia ya mtandao , wakiomba tunawachukua na kuwapeleka kwenye vituo maalumu, tunaenda kuwafundisha kilimo biashara kwasababu kwa muda mrefu tumekuwa tukitazama kilimo kama sehemu ya maisha , lakini hivi sasa heka moja ya mtu ndio duka lake, ndio kiwanda chake , kwa hiyo tunakwenda kuwafundisha biashara kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka minne bila kulipa gharama yoyote , atalala bure, atakula bure.Akishafundishwa tunakwenda kumpa kipande cha ardhi kisichozidi heka 10,” Amesema Bashe.
Amefafanua kuwa kijana atapewa hati ya umiliki ya miaka 66 kwa hiyo kile kitendo cha taasisi za fedha kusema huyu kijana hana ardhi, hana dhamana kimeondoka , na wakati huohuo tunakuwa tumepima udongo unahitaji zao gani. Na mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan atazindua “Block Farm”ya kwanza yenye hekta 1000 katika Mkoa wa Dodoma ambayo itakuwa imechukua vijana , na hii ndio “Block Farm” ndogo nchini.
“Serikali imeamua kuweka mkakati wa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na kutegemea kilimo cha mvua za masika,” Amesema Bashe.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhuru Yunus amesema Rais Dkt Samia alipokuwa Senegal aliwaelezea washiriki kuwa watanzania wana utayari wa kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo kwa vitendo.
Katika mazungumzo hayo na wanahabari pia wamehudhuria Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Gerald Geofrey Mweli pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao, Wizara ya Kilimo, Nyasebwa Chimagu