Katibu Mkuu wa Chama Cha Democratic Party (DP)Abudul Mluya akizungumza kwenye kikao Cha ndani na wanachama wa chama hicho kuelekea kwenye uzinduzi wa mikutano yao ya hadhara
Mratibu wa Chama Cha Democratic Party Ayoub Sanga akitoa maelezo ya rangi zilizoko kweye Bendera ya Chama hicho kwa wanachama.
Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Taifa kutoka Chama Cha Democratic Party (DP) Felix Makuwa wapili ni Katibu Mkuu Abdul Mluya watatu ni Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Dkt.Paul Buzuka na wanne ni Mjumbe wa Chama hicho Emmanuel Nzagamba
Lameck Khamis akipokea Kadi ya uanachama wa Chama Cha Democratic Party kutoka kwa Katibu Mkuu wa DP Abdul Mluya.
Elizabeth Lufungulo akipokea Kadi ya uanachama wa Chama Cha Democratic Party kutoka kwa Katibu Mkuu wa (DP) Abdul Mluya
………………………………
Na.Hellen Mtereko-MWANZA
Chama Cha Democratic Party (DP) kimesema kinahitaji Katiba bora itakayokidhi matakwa ya watanzania na ustawi wa Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Jumamosi Januari 28,2023 na Katibu Mkuu wa (DP) Abudul Mluya
wakati akizungumza na Viongozi,wanachama wa Chama hicho Mkoani Mwanza kuelekea kweye uzinduzi wa Mikutano ya hadhara.
Amesema hoja yao ni kuwa na katiba bora nasiyo mpya ambayo itawanufaisha watawaliwa na watawala.
” Hata Muwasisi wa Chama Cha Democratic Party Marehemu Mtikila alikuwa akisisitiza Katiba bora na siyo Katiba mpya kwa maana ya kubadilisha maandishi na jalada”, amesema Mluya
Mluya amesema tayari wameishaanza mikakati ya kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa huku akiwaomba viongozi kwenda kuandaa wagombea udiwani na wabunge kwenye maeneo yao.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa DP Mkoa wa Mwanza Dkt.Paul Buzuka, amesema wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafanya mikutano yenye tija ambayo itakuwa ni chachu ya kuwaletea maendeleo Watanzania.
Akisoma madhumuni ya Chama hicho Mwenyekiti wa DP Mkoa wa Mara Chrisant Nyakitita, amesema ni kuwasaidia Wananchi katika kuhakikisha kunakuwepo na Demokrasia nchini,kujenga upya jamii yenye maadili safi na katika msingi bora wa elimu kwa watoto,vijana na wazee watakaoiwezesha nchi kwenda na wakati wa kimaendeleo pamoja na kufufua,kuinua uchumi wa nchi na kurejesha njia zote kuu za uchumi.
Rebecca Buzuka na Lameck Khamis ni wanachama wa (DP) wamesema kuanza kwa mikutano ya hadhara ni jambo zuri ambalo litawasaidia kuwafikia wananchi kwaajili ya kusikiliza kero zao.