Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikata keki kama ishara ya kumbukizi ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro – Swaswa. Kiasi cha shilingi Milioni 92.8 zimepatikana katika hafla ya kuchangia gharama za masomo wanafunzi wenye uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza katika katika hafla ya kumbukizi ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro – Swaswa. Kiasi cha shilingi Milioni 92.8 zimepatikana katika hafla ya kuchangia gharama za masomo wanafunzi wenye uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara. Wanafunzi hao ni wa ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada)
…………………….
Mkoa wa Dodoma umeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha matukio makubwa matatu ya kimkakati ambayo yameweka kumbukumbu ya kudumu kwa jamii na matokeo chanya Matukio hayo ni pamoja na changizo la kugharamia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, uzinduzi kwa kituo jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na zoezi la upandaji miti.
Kiasi cha shilingi Milioni 92.8 zimepatikana katika chakula cha hisani kilichoandaliwa maalumu kusheherekea siku ya kuzaliwa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuchangia gharama za masomo wanafunzi wenye uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika hafla ya kuchangia Mfuko wa Kichungaji wa Elimu Mtwara (Mtwara Pastoral Education Fund – MPEF) ametoa rai kwa jamii kuhakikisha wanawezesha wanafunzi wahitaji kusoma ili kufikia ndoto zao.Katika hafla hiyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 50 huku milioni 42.8 zikichangwa na wageni walioalikwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua kituo cha utoaji huduma jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kilichopo hapa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Akizindua kituo hicho Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma ni kati ya Mikoa yenye changamoto za matukio ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto, hivyo kituo hicho cha kwanza katika Mkoa kitasaidia manusura wa ukatili ambao watapata huduma zote kwa haraka kwa wakati muafaka.
Amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ni kurahisisha mfumo wa rufaa kwa manusura katika kupata huduma maalumu zingine kama vile huduma za afya, Ustawi wa Jamii na huduma za msaada wa kisheria.
“Hakikisheni kituo hiki kinafanya kazi masaa 24 ili kurahisha huduma na kutumiza malengo ya uanzishwaji wake” Alisisitiza Mhe. Senyamule.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alijumuika na jumuiya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika zoezi la upandaji miti takribani 400 katika eneo la Vikonje ambapo makao makuu ya TBC yanajengwa.