……………………
Na Mwamvua Mwinyi, Rufuji
Januari 28
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa kamati Kuu,Fadhil Maganya ameendelea na ziara yake Mkoani Pwani ambapo Januari 28,amezindua jengo la Mionzi , hospital ya Utete wilayani Rufiji ambalo limegharimu milioni 140 hadi kukamilika kwake.
Akizindua jengo hilo,Maganya ametoa wito ,kutunzwa kwa Raslimali hiyo na vifaa vilivyopo .
Aliwaasa watumishi wa afya ,kutoa huduma bora kwa wagonjwa na Kuwa na lugha nzuri badala ya kutoa lugha chafu inayokatisha tamaa .
“Serikali inafanya jitihada kubwa kuboresha huduma mbalimbali zikiwemo za afya ,inatumia fedha nyingi hivyo majengo haya yatunzwe na kulindwa ili yadumu “
“Nimshukuru na kumpongeza Rais wetu,Samia Suluhu Hassan na Januari 27 ilikuwa siku yake ya kuzaliwa,mungu azidi kumpa maisha marefu ,aendelee kutuongoza na sisi kazi yetu ni kumuunga mkono kwa makubwa anayoyafanya katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi”alisema Maganya.
Awali mganga mfawidhi wa hospital hiyo, dkt.Ephrem Tahhani aliishukuru Serikali kwa kutoa mtambo wa Mionzi wenye thamani ya milioni 180 .
Alieleza jengo la Mionzi limegharimu milioni 140 Hadi kukamilika kwake,na kusema milioni 137 imetumika kwa ajili ya manunuzi ya vifaa mbalimbali vya ujenzi pamoja na malipo ya fundi na milioni 2.4 kwa ajili ya matazamio ya mradi.
Ephrem alieleza, Mradi huyo utasaidia kupata huduma hiyo ya karibu kwa Wananchi ambao kwa miaka mingi walikuwa wakifuata huduma hiyo umbali wa km 70 nje ya wilaya.
Katika ziara hiyo pia ,Maganya ametembelea ,chemchem ya maji moto Utete ambayo mwaka 1905 imegundulika na Mtanganyika Adrahman Mchuchuli huku,kisima kikiwa kimejengewa 1945 na Waingereza.
Mwisho