Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akifungua kikao kazi Cha majadiliano kuhusu rasimu ya Muswaada mpya wa bima ya Afya Kwa wote unaotarajiwa kupelekwa na kusomwa Kwa mara ya kwanza bungeni kilichofayika kwenye jengo la watoto Katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kati ya wahariri wa vyombo vya habari za Wizara.
Mkurugenzi Mkuu wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw.Bernald Konga akifafanua baadhi ya mambo yanayohisu rasimu ya muswaada huo wakati wa majadiliano Katika kikao kazi hicho kati ya Wizara na wahariri wa vyombo vya habari.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Profesa Abel Mkubi akijibu baadhi ya maswali ya wahariri wa vyombo vya habari waliotaka ufafanuzi kuhusu mambo kadhaa yaliyomo Katika rasimu hiyo ya muswaada wa Bima ya Afya Kwa wote.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA Dkt. Bagayo Saqware akijibu baadhi ya maswali ya wahariri.
Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile mara baada ya kufungua kikao kazi Cha majadiliano kuhusu rasimu ya Muswaada mpya wa bima ya Afya Kwa wote.
Baadhi ya picha zikionesha wahariri wa vyombo vya habari na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya wakiwa kwenye kikao hicho
…………………………………
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Waziri wa Afya Ummy mwalimu amesisitiza umuhimu wa bima ya Afya kwa wananchi ambapo amesema kwa sasa serikali kupitia Wizara ya Afya ipo katika hatua za kufungamanisha Bima ya Afya na huduma zingine.
Kuhusu toto Afya kadi Waziri ameeleza kwamba bima ilionekana kuwa na manufaa makubwa kwani asilimia kubwa ya watoto huwa hawaumwi mara kwa mara ambapo ilikuwa elfu 50 mia nne lakini imeonekana kuwepo kwa mzigo mkubwa kwenye huduma za kadi ya bima hiyo kwamba mtoto anachangia elfu hamsini mia nne(elfu50400) matumizi yake yanakuwa mara mia tatu ndio maana serikali kupitia Wizara imeamua kufungamanisha ili hata wasiokuwa wepesi wa kuingia kwenye bima waingie.
Ni lazima kuwa na bima ya Afya lakini sio kosa la kisheria kwa kutokuwa na Bima ya hiyo, hakuna mtanzania atakamatwa wala kufugwa kwa kukosa Bima Afya,
Amesema Waziri Ummy.
Waziri Ummy ameongeza kwamba Bima ya Afya si jambo rahisi mfano nchi kama Marekani wamejadili suala la hilo kwa miaka mingi na kwa sasa kwao Bima ya Afya ni lazima kwa kila mwanachi.
Aidha ameongeza kwamba yupo tayari kupokea maoni na ushauri kwa wahariri na wananchi ili waendelee kuboresha jeduali la marekebisho kuhusu mjadala mzima wa Bima ya Afya kwa wote.