Wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari inatarajia kupeleka mswada wa huduma za habari kwa ajili ya marekebisho ya sheria ya habari mwezi wa kwanza 2023 katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jukwaaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alisema kuwa macho na masikio ya wadau wa habari nchini, yanaelekezwa jijini Dodoma kusubiri muswada wa Sheri ya Habari ukisomwa kwa mara ya kwanza Januari hii.
Balile alisema kuwa mwezi huu wa kwanza wanategemea wizara ya habari,mawasiliano na teknolojia ya habari itawasilisha huo mswada wa huduma za habari kwa ajili ya wadau wa habari.
Alisema kuwa kupitishwa kwa mswada wa huduma za habari kutasaidia kupatikana kwa sheria ya huduma ya vyombo vya habari ambao utasaidia kuunda kwa Baraza huru la habari.
Balile alimazia kwa kusema kuwa kupelekwa kwa mswada huo bungeni maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan yatakuwa yametekelezwa kwa faida ya wadau wa habari nchini.