Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akifungua kikao kazi cha kamati yake jijini Dodoma, kilichopokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kipindi cha nusu mwaka cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2022.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha nusu mwaka kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Denis Londo akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo jijini Dodoma, kilichopokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha nusu mwaka cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2022.
Sehemu ya Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Denis Londo (hayupo pichani) wakati akiwasilisha hoja kwenye kikao kazi cha kamati yake, kilichopokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kipindi cha nusu mwaka cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2022.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Tunza Malapo akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo jijini Dodoma, kilichopokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha nusu mwaka cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2022.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifafanua hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na ofisi yake jijini Dodoma, kilichopokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha nusu mwaka cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2022.