Mwakilisi wa mkurugenzi wa Wakala wa Usalama wa Chakula TFDA Mwambole Bw. Lazaro akizungumza katika mkutano huo.
Denis Nyakisinda mwakilishi wa Katibu Tawala mkoa wa Mara akizungumza katika mkutano huo
Lilian Koko msindikaji wa chakula akichangia hoja katika mafunzo hayo.
………………………………………………………
Na Mussa John -Mara
Wasindikaji wa Wadogo wa chakula Mkoani Mara wamelalamikia upungufu wa vifungashio vya bidha zao wanazozalisha hapa nchini kutokupatikana kwa urahisi na hivyo kutokukidhi ubora wa kimataifa, na kuwalazimu kufata nchi jirani yakenya kwani imekuwa ikiepelekea bidhaa zao kukosa soko la ndani na Nje ya Nchi.
Rai hiyo imetolewa na wasindikaji hao katika warsha ya siku mbili iliyo andaliwa na Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA)ambapo walikuwa wakipatiwa mafunzo yanayolenga kuongeza usalama wa chakula pamoja na kuwa na viwango vya kitaifa na kimataifa.
Akizungumza wakati wa warsha hiyo mwakilishi wa mkurugenzi wa usalamawa chakula (TFDA)Lazaro Mwambole alisema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajasiliamali wa mazao ya usindikaji ili kukidhi viwango vya kimataifa na kuwa na fursa katika masoko ya kimataifa.
Alisema mpaka sasa wameisha toa mafunzo hayo katika mikoa 26 ya Tanzania bara ili kuondoa changamoto za wafanyabiashara hao ambao wengi wamekuwa wakifanya shuguli zao kwa mazoea na bila ya kujali viwango vinavyo tolewa na TBS.
Mwambole alisema kuwa wajasiliamali wengi wa mazao ya kusindika wanakabiliwa na kutokuwa na usajili kutoka Mamlaka ya chakula na dawa na kufanya viwanda vingi vya usindikaji kuwa majumbani mwa wajasiliamali hao jambo ambalo husababisha hata viwanda hivyo vidogo kushidwa kukidhi matakwa ya usafi.
Kwaupande wake kaimu katibu tawala wa Mkoa Dennis Nyakisinda alisema kuwepo kwa viwanda vidogo vya usindikaji kunachangia kukuza pato la mtu moja moja na kuongeza pia pato la taifa lakini kuwezesha pia Tanzania kuweza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Alisema shuguli za usindikaji pia zinaweza kuwa ni sehemu ya kuangamiza jamii kutokana na kula chakula kilicho sindikwa bila ya kuzingatia ubora wa usindikaji kwani badala ya kuleta nafuu kwa watumiaji yaweza kuwa ni chanzo cha magonjwa mengine.
Nyakisinda aliongeza kusema kuwa wajasiriamali hao wanapaswa kuzingatia mafunzo hayo walio pewa kwa lengo la kuongeza thamani katika bidhaa zao na kuweza kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi kwa ujumla.
“ usindikaji mbaya wa vyakula na mazao ni chanzo cha magonjwa katika jamii kama mazao yasipo sindikwa vizuri yanaweza kusababisha kuwepo kwa sumu kuvu ndani yake na malaji anapo tumia tayari anapata madhara ” alisema.
Nae kaimu meneja wa Mamlaka ya chakula na dawa kanda ya ziwa Mashariki Nuru Mwasulama alisema mpango huu wa kutoa elimu na kurasimisha wajasiliamali wa bidhaa za usindikaji ulitoholewa kwenye mpango wa miaka mitano ya taifa wa kuwezesha Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati lengo ni kuweza kuwafikia wafanya biashara wote wadogo nchini.
Alisema lengo kuu la tfda ni kuhakikisha walau asilimia 10 ya wajasiriamli walio pata mafunzo haya wanarasimishwa na kuingia katika mfumo wa ubora wa viwango na kupewa vyeti vya utambuzi kwa mwaka huu wa fedha wa 2018/2019.
Kwa upande wa wafanyabiashara za kusindika chakula na mazao mkoani hapa walikuwa na haya William Mnyasi alisema changamoto kubwa inayo wakabili ni kupata usajili wa bidhaa ambazo wanazizalisha pamoja na kupata nembo ya bidhaa .
Aliiomba mamalaka hiyo kuwapatia elimu ya mara kwa mara wasindikaji ya namna ya usindikaji bora ambayo yatawasaidia katika kuleta ufanisi wa bidhaa zao na kufanya usindikaji ulio bora na wenye kuleta afya njema kwa mtumiaji bila ya madhara yoyote.
Naye Lilian Koko ni msindikaji wa wine,jam,na mbilimbi alisema changamoto kubwa wanaipata ni katika vifungashio vya bidhaa zao visivyo na ubora ambapo alisema hapa nchini kuna vifungashio vya chupa nyenye mifuniko ya plastiki abayo ikika na bidhaa mda mrefu zinavujisha bidhaa hiyo na kushindwa kukisndana na bidhaa nyingine.
Alisema vifungashio vizuri na vyenye mifuniko ya bati ambapo kwa hapa nchini havipo mka nchi jirani ambapo mfanya biashara akivifta ili kuongeza samani ya bidhaa yake anakutana na changamoto ya bei anaponunua na mlindikano wa kodi anapo vipitisha mpakani hivyo kusababisha kushindwa kuendana naushindani wa kibiashara .