Waziri wa Nchi ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Jenista Mhagama pamoja na viongozi mbalimbali wakikata utepe kuashiria kuzindua mfuko wa Faida Fund kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo januari 14, 2023, Mfuko huo umeanzishwa na shirika la Watumishi Housing Ivestment ambalo ni shirika la Umma.
…………………………………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama amemkabidhi mfuko wa Faida Fund ambao uko chini ya shirika la Watumishi Housing Investment Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu Mwamba.
Waziri Mhagama amekabidhi mfuko Faida Fund katika uzinduzi rasmi wa mfuko huo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo januari 14,2023 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wageni waalikwa na wawekezaji walihudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Amesema Dkt. Natu Mwamba ni katibu mkuu mpya na mbobezi katika masuala ya kiutendaji na mnajua wanawake hawashindwi ila pia sijasema wanaume wanashindwa, ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ninakupongeza na ninampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukuteua hongera sana.” Amesema Mh. Jenista Mhagama.
“Nakukabidhi rasmi mfuko huu wa Faida Fund pamoja na kwamba sisi wote tunauangalia ila kwakuwa wewe ndiye unausimamia sasa ukimsaidia Mh. Waziri wa fedha naomba nikukabidhi mfuko huu awe mtoto wako umlee wewe mwenyewe na leo uanze na mtoto huyo wa “Faida Fund” nina imani mfuko huo utakuwa salama zaidi,” amesema Mh. Jensta Mhagama
Akizungumza kuhusu shirika hilo katika ujenzi wa nyumba za watumishi amepongeza Taasisi ya Watumishi Housing Investment kwa kufanikisha kujenga nyumba 983 Katika mikoa 19 Nchini ambazo zimeuzwa Kwa watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya Jamii.
Waziri Mhagama amesema kuwa Kwa kutumia mifuko ya hifadhi ya Jamii watumishi wa umma wameweza kupatiwa makazi ya kudumu hasa kwa kutumia mishahara yao kununua makazi hayo kwa muda mrefu na hivyo kuwapa uhakika pindi wanapostaafu sambamba na wale ambao wamekwisha staafu kuendelea kuishi katika makazi ya kudumu.
“Tumefurahi sana kuhamasishwa katika kipindi hiki cha miaka nane ambapo taasisi hii ya Watumishi Housing Investment toka ilipoanza imeweza kujipambanua katika katika kufanya kazi nyingi na zenye kuonekana”amesema Waziri Mhagama
Aidha Waziri Mhagama amesema kuwa Watumishi Housing wameendela kuhakikisha wanarahisisha namna ya kufanya malipo ya Nyumba hizo ziwe za kufika kwa wateja wote kwa taratibu mbalimbali ambazo wameziandaa.
Awali akizungumza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Natu Mwamba amesema kuwa ndoto za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuweza kuwawezesha wananchi mmoja kufikia uchumi Mzuri.
Amesema uuzaji wa vipande wa Mfuko wa Faida Fund ulioanza Mwezi Novemba Mwaka Jana hadi Disemba 31 umesaidia wawekezaji 3400 walijiandikisha ambapo kati ya hao 740 walishaanza tayari kuwekeza.
Dkt Natu amesema kuwa muitikio kutoka kwa wawekezaji wadogo,na wakati na Taasisi ikiwa ni pamoja na sekta ya Fedha imeendelea kufanya Mfuko huo kupata imani kwa wawekezaji.
Pia ametumia fursa hiyo kutoa wito Kwa Watumishi Housing Investment kuendelea kukuza Mfuko huo Kwa kutoa mafunzo stahiki ili uweze kuenea Nchini kote na kuwanufaisha wananchi na kukidhi matarajio kwa wadau wote.
Hata hivyo amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kushirikiana na Wananchi Housing Investment Pamoja na wadau wengine katika kendelea kujenga Mazingira bora ya uwekezaji katika kujiongezea kipato na Kupambana na umaskini.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Jenista Mhagama pamoja na viongozi mbalimbali wakishangilia mara baada ya kukata utepe kuashiria kuzindua mfuko wa Faida Fund kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo januari 14, 2023, Mfuko huo umeanzishwa na shirika la Watumishi Housing Ivestment ambalo ni shirika la Umma.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Jenista Mhagama akizungumza wakati akizindua mfuko wa Faida Fund kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Deodatus Ndejembi akimkaribiaha Waziri Jenista Mhagama ili kuzindua mfuko huo
Mkurugenzi Mtendaji CMSA CPA Nicodemus Mkama akizungumza kabla ya uzinduzi huo uliofanyika leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investmet Dkt Fredy Msemwa akitoa maelezo kabla ya uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investmet Dkt Fredy Msemwa akitoa maelezo kabla ya uzinduz huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Brass Band ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT ikiwaongoza watumisi wa shirika la Watumishi Housing Imvestiment wakati wakiingia kwa maandamano kwenye kumbi wa Julius Nyerere.
Brass Band ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT ikiwaongoza watumisi wa shirika la Watumishi Housing Imvestiment wakati wakiingia kwa maandamano kwenye kumbi wa Julius Nyerere.
baadhi ya wafanyakazi wa Watumishi Housing Investment wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investmet Dkt. Fredy Msemwa akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya leo kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali zikionesha wakuu wa mashirika na waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.