Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu (kushoto mwenye shati jeupe) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) pia akiwemo Diwani wa Kata ya Minazi mirefu Godlisten Malisa.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu akikagua gwaride maalum la vijana wa kata ya Minazi Mirefu wakati wa mapokeo kwenda kwenye ziara.
Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu jimbo la Segerea jijini Dar es salaam Goldsten Malisa (katika) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Saidi Sultan Side (kulia) pamoja na mwanachama wa CCM (kushoto)
Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu jimbo la Segerea jijini Dar es salaam Goldsten Malisa wakiwa katika jengo la SUDECO akimueleza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu dhamira yao ya kulihitaji eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu, Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu jimbo la Segerea jijini Dar es salaam Goldsten Malisa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Saidi Sultan Side pamoja na wananchama wa CCM wakiwa katika eneo la majengo ambayo yako chini ya umiliki wa Mamlaka Ya Hali Ya Hewa (TMA).
Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu jimbo la Segerea jijini Dar es salaam Goldsten Malisa (kushoto) pamoja na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea,Lutta Rucharaba wakizungumza na wanahabari walioshiriki kwenye ziara hiyo.(picha na Mussa Khalid)
…………………….
NA MUSSA KHALID
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu ameahidi kulifuatilia suala la uwepo wa majengo yasiyotumika katika Kata ya Minazi Mirefu jijini Dar es salaam ili serikali itoe kauli kama itayatumia au yarudishwe kwenye Halmashauri yaweze kujengwa kituo cha Afya pamoja na Shule.
Naibu Spika Zungu ametoa kauli hiyo mapema leo jijini Dar es salaam baada ya kufanya ziara katika kata hiyo ya kuyatembelea majengo ya SUDECO yaliyokuwa yanamilikiwa na wizara ya kilimo na hali ya hewa ambayo yako chini ya umiliki wa Mamlaka Ya Hali Ya Hewa (TMA).
Amesema kuwa majengo hayo ni ya serikali lakini yametelekezwa kwa muda mrefu hivyo atahakikisha analifuatilia hilo ili majengo hayo yaweze kutumika katika kuwahudumia wananchi kwa kujengwa kituo cha Afya na Shule.
‘Nimepokea Maombi yenu na mimi nitalifanyia kazi ili serikali itoe kauli yake kuhusu majengo haya kwani nimeambiwa kuwa kata hii haina shule ya msingi na wala haina kituo cha Afya na wananchi wengi wanateseka kupata huduma za afya hivyo nafahamu kwamba serikali yetu ni sikivu italishughulikia swala hilo’amesema Naibu Spika Zungu
Aidha Naibu Spika Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala jijini Dar es salaam amesema kuwa serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluh Hassan inafanya kazi kwa ueledi hivyo miradi hiyo ni lazima isemewe ili wananchi waendelee kuwa karibu na serikali yao.
Awali akizungumza Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu jimbo la Segerea jijini Dar es salaam Goldsten Malisa amesema kuwa kufanikisha kupata majengo hayo itasaidia kuwaondolea adha wananchi wa kata hiyo kwenda umbali mrefu kutafuta huduma.
‘Sababu kubwa ya Ujio wa Naibu Spika ni katika kuongeza nguvu ya kufanikisha maombi yao ya kupatiwa majengo ili kuweza kuwaletea wananchi wa Minazi Mirefu Shule na Kituo cha Afya’amesema Diwani Malisa
Kwa upande wake Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea,Lutta Rucharaba ametumia fursa hiyo kusema kuwa kwa ushirikiano wa Mbunge na Diwani utasaidia kufanikisha kupata maeneo hayo kwani serikali nisikivu.
Hata hivyo katika ziara hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Saidi Sultan Side pamoja na wanachama wa chama hicho.