Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), ametembelea na kujionea namna ujenzi wa jengo la Wizara katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma unavyoendelea.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi Mhe. Dkt. Tax amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kuongeza kasi ili ujenzi ukamilike kwa wakati.
“Nimetembelea hapa, nimejionea kazi ilipofika, kazi bado ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili Mungu akijaalia mwezi Oktoba mwaka huu badala ya Desemba ujenzi uwe umekamilika na tuone tunajipanga namna gani,” amesema Dkt. Tax.
Amesema Wizara ina uhitaji mkubwa wa jengo hilo kwa kuwa watumishi wametawanyika katika maeneo matatu tofauti na inakuwa ngumu kukutana kwa haraka pale inapobidi.
Amesema kukamilika kwa jengo Hilo kutatoa ahueni kwa watumishi wa wizara na kuwawezesha kuwa sehemu moja na hivyo kurahisisha utendaji kazi wa Wizara.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Dkt. Tax aliambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine na watendaji wengine wa Wizara.
Ujenzi wa jengo la Wizara ulianza mwezi Januari 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2023. Ujenzi huo utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 22.9 ambazo zimetolewa na Serikali ili kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.
Ujenzi huo unafanywa na Umoja wa makampuni ya Sole works na mshauri elekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 07 Januari 2023
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha wageni akiwa ameambatana na Mhe. Dkt. Tax kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 07 Januari 2023
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na wakandarasi wa jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambapo aliwahimiza kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akitoa taarifa fupi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara kwa Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Balozi Mbarouk walipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma
Sehemu ya Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamsikiliza Mhe. Dkt. Tax wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serijkali Mtumba
Sehemu ya Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamsikiliza Mhe. Dkt. Tax wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serijkali Mtumba
Kikao kikiendelea
Mhandisi wa Wizara, Bw. Kiswaga naye akitoa ufafanuzi kwa Mhe. Waziri Tax kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara
Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa Jengo la Wizara akitoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo ambapo kwa sasa limekamilika kwa asilimia 55.
Mkandarasi wa Jengo la Wizara akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt. Tax kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo kwa kuonesha picha
Mhe. Balozi Mbarouk akiangalia sampuli ya fremu za milango na kusisitiza ujenzi huo uzingatie ubora wa hali ya juu ya vifaa vyote.
Mhe. Balozi Mbarouk akisisitiza jambo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Wizara
Mhe. Dkt. Tax kwa pamoja na Mhe. Balozi Mbarouk wakiingia kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma
Mhe. Dkt Tax akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara
Mhe. Dkt. Tax akimsikiliza Mkandarasi wa Wizara, Bw. Kiswaga wakati akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya ujenzi wa jengo la Wizara
Mhe. Dkt. Tax akipanda ngazi kuelekea ghorofa za juu za jengo hilo ili kukagua maendeleo ya ujenzi
Mhe. Dkt Tax akiwa amekamilisha ukaguzi wa jengo la Wizara na kuwataka wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo.